HARMONIZE ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA
Msanii wa Bongofleva Harmonize hatimaye ameiweka wazi tarehe ya kuiachia album yake mpya iitwayo “High School”. Album hiyo ambayo ilipaswa itoke mwezi huu wa haitotoka kutokana na sababu mbalimbali hivyo imesogezwa mbele hadi Novemba 5 mwaka huu. Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mkali huyo wa “Teacher” ambao wanaisubiri “High School album” kwa hamu kubwa. Ikumbukwe, hii inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Harmonize baada ya “Afro East” iliyotoka mwezi Machi mwaka wa 2020.
Read More