Grace Mwai na mume wake Hiram Kamuhunjia wakiri kufanya maombi kabla ya tendo la ndoa

Grace Mwai na mume wake Hiram Kamuhunjia wakiri kufanya maombi kabla ya tendo la ndoa

Mtengeneza maudhui kutoka Kenya Hiram Kamuhunjia na mchumba wake mwimbaji wa nyimbo za injili Grace Mwai wamefichua kuwa huwa wanasali kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Wakizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu na wanandoa mashuhuri wa Akorino Carey Priscilla na Benito Muriu, wawili hao walisema hata Wakristo wanapaswa kufuata taratibu za kidini katika maisha yao ya ngono. “Unajua watu hawajui kuwa urafiki wa kimwili ni wa kiroho. Kwa hiyo tukiwa kwenye huo mchezo huwa tunaomba kila wakati. Tunaomba kwa sababu unapokuwa kwenye mchezo huo unaeza jipata umepoteza uja uzito, hivyo lazima uombe.”, Walisema. Hiram na Grace Mwai walihalalisha mahusiano yao kama wanandoa mapema mwaka huu.

Read More