Holy Dave akanusha tuhuma za kumshambulia mtu kwa chupa ya pombe

Holy Dave akanusha tuhuma za kumshambulia mtu kwa chupa ya pombe

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Holy Dave amekanusha madai ya kumjeruhi mtu kwa chupa ya pombe kwenye moja ya klabu ya usiku huko Kilimani, Nairobi. Akimjibu shabiki yake aliyemtupia maneno makali mtandaoni baada ya kutajwa kuhusika kwenye kashfa hiyo, Holy Dave amesema ameshangazwa na namna watu wanavyomhukumu bila kujua undani wa taarifa hiyo. Mwanamuziki huyo amesema madai ya kumpiga mtu na chupa hayana msingi wowote huku akisisitiza kuwa ukweli utabainika hivi karibuni. “Don’t be too quick to judge. There was no beer bottle or any bottle involved. The truth will come out,” Alisema Holy Dave. Wiki moja iliyopita Holy Dave alifikishwa katika mahakama ya Kibera kujibu mashtaka yaliyoibuliwa dhidi yake ya kumjeruhi, jamaa aitwaye Keem David na chupa ya pombe, akimuacha majeraha mabaya mwilini. Hata hivyo alikana mashtaka yote mbele ya mahakama ambapo aliachiwa huru kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ugomvi wao.

Read More
 Holy Dave aburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi mtu na chupa ya pombe

Holy Dave aburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi mtu na chupa ya pombe

Msanii wa injili nchini Kenya Holy Dave amefikishwa katika mahakama ya Kibera kwa madai ya kumpiga kichwani mfanyabiashara moja kwa kutumia chupa ya pombe katika klabu ya usiku huko Kilimani, Nairobi. Holy Dave ambaye aliachiwa kwa dhamana , alikana mashtaka ya kumshambulia Keem Daudi na kumsababishia majeraha mabaya mwilini. Hata hivyo wapelelezi wa kesi hiyo wamefanikiwa kuzipata picha za CCTV ambazo zitatumika kama ushahidi katika kesi hiyo. Mahakama ilifahamishwa kuwa mnamo Oktoba 1, mwaka 2022, Holy Dave alimshambulia mwathiriwa baada ya kuingia kwenye ugomvi alipokuwa akimtetea rafiki yake ambaye alitaka kujiunga naye katika sehemu ya watu mashuhuru klabuni hapo lakini alikuwa akizuiwa na walinzi.

Read More