Mwanamuziki kutoka Kenya Hopekid ajizawadi gari mpya aina ya Mercedes Benz

Mwanamuziki kutoka Kenya Hopekid ajizawadi gari mpya aina ya Mercedes Benz

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Hopekid ameamua kutumia ipasavyo pesa ambazo anazitolea jasho Hii ni baada ya kujizawadi gari aina Mercedes Benz kutokana na mafanikio ambayo ameyapata kupitia muziki wake. Kupitia ukurasa wake instagram amechapisha picha ya gari yake mpya na kusindikiza na ujumbe unaosomeka “Allow me to celebrate my small wins with you ☺️😊☺️ let me bless ur TL with my brand new merc.” Hata hivyo mashabiki pamoja na mastaa wenzake wamempongeza kwa mafanikio hayo huku wakimtakia kila la heri katika siku za mbeleni.

Read More
 HOPEKID MBIONI KUFUNGUA STUDIO YAKE YA MUZIKI

HOPEKID MBIONI KUFUNGUA STUDIO YAKE YA MUZIKI

Hitmaker wa ngoma ya “Holiday”, Msanii Hope Kid amedokeza mpango wa kuzindua studio ya kurekodi muziki iitwayo Autism Lights. Katika mahojiano yake hivi karibuni Hopekid amesema studio hiyo ya muziki itakuwa mahususi kwa ajili ya kukukuza vipaji vya watoto wenye changamoto ya usonji (Autism). Katika hatua nyingine Hope Kid pia ametusanua kuwa Juni 20 mwaka huu, watatembelea makazi ya watoto walioathirika na usonji ambapo watatoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine ya msingi, msaada ambao utawasaidia kujikimu kimaisha katika kipindi cha miezi 6 ijayo. Usonji ni hali ambayo mtu huwa nayo tangu utotoni ambayo hutambulika kwa mhusika kushindwa kuwasiliana vizuri na pia kujihusisha na watu wengine katika mambo mbalimbali ya kijamii katika hali ya kawaida.

Read More