Colonel Mustafa Adai Kuwasaidia Huddah na Noti Flow Kufikia Umaarufu

Colonel Mustafa Adai Kuwasaidia Huddah na Noti Flow Kufikia Umaarufu

Msanii mkongwe wa muziki nchini Kenya,Colonel Mustafa, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa muda aliowahi kutumia na mastaa wa kike kama Huddah Monroe na Noti Flow uliwasaidia kupenya kwenye anga la umaarufu, wakati walipokuwa bado hawajatambulika sana katika tasnia ya burudani. Akizungumza kwenye podcast ya Alex Mwakideu Live, alisema kwamba mahusiano yake na wanawake hao yalimsaidia kuwapa mwanga wa mafanikio waliokuwa bado hawajaufikia kwa wakati huo. Kwa mujibu wa msanii huyo, jina lake lilihusishwa na mastaa hao kabla ya wao kung’aa, na hivyo mchango wake haupaswi kupuuzwa. Kauli hiyo imeibua hisia mseto mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa Mustafa alikuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya Huddah na Noti Flow, huku wengine wakimtuhumu kwa kujitafutia kiki na kutumia majina ya watu maarufu kurudi kwenye ramani ya burudani. Hadi sasa, Huddah Monroe na Noti Flow hawajajibu madai hayo, lakini mashabiki wanazidi kufuatilia kwa makini endapo wahusika watajitokeza kuweka wazi upande wao wa simulizi hii. Mustafa, anayekumbukwa kwa kazi zake akiwa na kundi la Deux Vultures, anaonekana kurejea tena kwenye vyombo vya habari si kwa muziki, bali kwa matamshi yenye utata kuhusu mahusiano ya zamani.

Read More
 Huddah Monroe Ataka Roboti Badala ya Watu, Alalamikia Uzembe Kazini

Huddah Monroe Ataka Roboti Badala ya Watu, Alalamikia Uzembe Kazini

Mjasiriamali na mwanasosholaiti maarufu wa Kenya, Huddah Monroe, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kulalamikia wafanyakazi wake kwa kile alichokitaja kama kukosa akili ya kawaida (common sense) katika kushughulikia mambo madogo kazini. Katika ujumbe wake uliojaa malalamiko na kejeli kupitia InstaStory, Huddah alieleza kukerwa na kile alichokiita uzembe na ukosefu wa ufanisi, kutoka kwa wafanyakazi wa ngazi ya juu hadi chini. Alisisitiza kuwa hana tatizo na kazi kubwa, bali ni mambo madogo kama usafi na uangalifu wa mazingira ambayo yanamvunja moyo zaidi. “Nina timu nzima, lakini hakuna anayefikiria kuondoa maua yaliyoanza kuoza mezani. Nitafungua duka la kwanza la roboti Kenya!, Nahitaji clone (nakala yangu) kwa sababu timu yangu haiwezi hata kushughulikia mambo madogo,” aliandika Huddah, akionyesha wazi kutoridhika na utendaji wa kikosi chake cha sasa. Kauli hiyo imezua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake, baadhi wakimuunga mkono kwa kutaka nidhamu kazini, huku wengine wakimkosoa kwa lugha ya ukali dhidi ya wafanyakazi wake. Wapo pia waliodokeza kuwa kauli yake inaonyesha shinikizo kubwa analokumbana nalo katika kuendesha biashara. Huddah, anayejulikana kwa ujasiriamali wake na uwazi katika mitandao ya kijamii, amekuwa mstari wa mbele kukuza bidhaa za urembo chini ya chapa ya Huddah Cosmetics, na pia hujulikana kwa mtindo wake wa maisha wa kifahari. Hadi sasa, hajatoa taarifa nyingine kufuatia malalamiko hayo, lakini ujumbe wake umeonyesha wazi kuwa anataka mabadiliko ya haraka katika timu yake – au roboti wachukue usukani.

Read More
 Huddah Monroe: Wanaume wa Gen Z Hawana Ujasiri wa Kuwatongoza Wanawake

Huddah Monroe: Wanaume wa Gen Z Hawana Ujasiri wa Kuwatongoza Wanawake

Mfanyabiashara na mwanasosholaiti maarufu kutoka Kenya, Huddah Monroe, amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu wanaume wa kizazi cha Gen Z. Kupitia mitandao ya kijamii, Huddah alisema kuwa wanaume wa kizazi hiki wamekosa ujasiri wa kutangamana na wanawake na kuanzisha mazungumzo, tofauti kabisa na enzi za Millennials. Huddah alieleza kushangazwa na tabia ya wanaume wa kizazi cha Gen Z ambao, kwa mtazamo wake, huonekana kuogopa au kutojihusisha moja kwa moja na wanawake katika mazingira ya kijamii.  “Navaa ninja yangu na kwenda sehemu za kijamii kwa ajili ya utafiti wangu tu, maana sina ninayemtaka huko. Lakini wanaume hawakaribii wanawake,” aliandika Huddah. Huddah aliendelea kueleza kuwa hali hiyo imemfanya awahurumie wanaume wa kizazi hiki kwa sababu mawasiliano ya ana kwa ana yamepungua sana. Kwa maoni yake, kizazi cha sasa kinaonekana kuwa na uwoga au labda kimezidiwa na matumizi ya mitandao ya kijamii, kiasi cha kushindwa kuwa na ujasiri wa kawaida wa kuanzisha mazungumzo. “Millennials walikuwa na game. Gen Z wanaonekana kama wamekata tamaa. Wengine wakijaribu, mazungumzo yao hayana ladha wala mvuto,” aliongeza. Kauli hii imechochea maoni mbalimbali, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa kusema anasema ukweli mchungu. Wengine wamehusisha hali hiyo na mabadiliko ya kijamii, hofu ya kukataliwa, au ongezeko la mtazamo hasi dhidi ya wanaume wanaowakaribia wanawake bila mwaliko. Huddah, ambaye ana sauti kubwa mitandaoni kuhusu masuala ya kijamii, anasema hali hii inaweza kuwa ishara ya matatizo makubwa zaidi katika namna watu wa kizazi kipya wanavyojenga mahusiano.

Read More
 Huddah Monroe Afichua Alikuwa Ameolewa kwa Miaka 4, Lakini Ndoa Ilivunjika Mwaka Jana

Huddah Monroe Afichua Alikuwa Ameolewa kwa Miaka 4, Lakini Ndoa Ilivunjika Mwaka Jana

Sosholaiti maarufu kutoka Kenya, Huddah Monroe, amewashangaza mashabiki wake baada ya kufichua kuwa aliwahi kuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka minne. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Huddah alifichua kuwa aliishi maisha ya ndoa kwa siri, jambo ambalo halikujulikana na wengi. Katika ujumbe alioweka, Huddah alisema: “Nashukuru kwa kufanya mambo yangu kimya kimya. Nilikuwa nimeolewa kwa miaka minne mfululizo. Mwaka jana ilibidi tu iishe kwa sababu niligundua haikuwa sahihi. Nilichagua amani kuliko uhusiano wowote.” Kauli hii imezua gumzo mitandaoni huku wengi wakimsifia kwa ujasiri wa kuamua kuchagua amani na furaha yake binafsi. Ingawa hakufichua jina la aliyekuwa mume wake, Huddah aliweka wazi kuwa maisha ya ndoa si rahisi kila wakati, na wakati mwingine ni muhimu kujitathmini na kuchukua hatua kwa ajili ya ustawi wa kiakili na kihisia. Huddah amekuwa akiishi maisha ya faraghani kwa muda sasa, tofauti na kipindi cha nyuma ambapo alikuwa maarufu kwa mitindo ya maisha ya kifahari na mijadala mitandaoni. Sasa anaonekana kuzingatia zaidi maisha ya binafsi na biashara zake. Kauli yake inaibua mjadala kuhusu umuhimu wa amani ya ndani katika mahusiano, na kwamba si kila uhusiano unaofikia mwisho ni wa kushindwa — bali wakati mwingine ni ushindi wa binafsi.

Read More
 Siwezi kuolewa na mwafrika, nataka mrusi – Huddah Monroe

Siwezi kuolewa na mwafrika, nataka mrusi – Huddah Monroe

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amesema kamwe hatokuja kuolewa na Mwafrika kwa sababu ataendelea kuteseka na umaskini. Huddah alisema kuwa kama kuna mwanaume ambaye atakubali kumtolea posa bila kupepesa, ni Mrusi. Kwa mujibu wa Huddah, bara zima la Afrika halina musitakabali angavu na kutwa kucha ni kuhangaika na umaskini, jambo ambalo hakuumbiwa yeye. “Mustakabali wa Afrika si angavu hata kidogo asikudanganye mtu. Nataka mwanamme wa Urusi haraka iwezekanavyo. Siwezi olewa na Mwafrika kwa sababu tutaendelea kujigaragaza katika mateso yale yale ya bara la Afrika,” Huddah aliandika. Huddah ambaye kwa muda mrefu amekuwa akionesha chuki yake kwa nchi yake Kenya na Waafrika wote hadharani aliwahi nukuliwa akisema kuwa yeye hutumia muda mwingi nje ya nchi kama vile Dubai katika kile alisema kuwa Kenya hakuna sehemu nzuri za kujivinjari na huwa hajihisi salama akiwa Kenya.

Read More
 Huddah Monroe mbioni kuzindua kitabu chake

Huddah Monroe mbioni kuzindua kitabu chake

Mrembo maarufu nchini, Huddah Monroe amedokeza kwamba hivi karibuni ataandika kitabu chake ambacho kitawasaidia watu kuhusu biashara. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kwamba kitabu hicho kitakuwa na masomo ya kutosha kuhusu jinsi ya kufanikiwa kibiashara na aliwahakikishia mashabiki wake kuwa watapenda kile ambacho atazungumza. “Siku moja nitaandika kitabu changu cha biashara, mtajua kuwa nachukia video, kwa hivyo maarifa yote utalazimika kupata kutoka kwenye kitabu sababu nitamwaga udaku mwingi kuhusu biashara na mahusiano ya kibiashara” amesema Huddah Monroe. Katika hatua nyingine, hivi karibuni, Huddah amekuwa akionekana kutokuwa sawa kiakili na mpaka kudokeza kuwa hayuko katika hali yake ya kawaida. Hii ni baada ya madai kuwa mwanasosholaiti huyo ni mjamzito kufuatia picha aliyopakia Instagram, madai ambayo alijitokeza kukana na kusema umbo la tumbo lilisababishwa na nguo kubwa aliyokuwa amevaa.

Read More
 HUDDAH AMCHANA RIHANNA NA WANAWAKE WANAOWAKIMBIA WATOTO KWA AJILI YA STAREHE

HUDDAH AMCHANA RIHANNA NA WANAWAKE WANAOWAKIMBIA WATOTO KWA AJILI YA STAREHE

Mwanamitindo na mjarisimali Huddah Monroe amemtolea mvivu mwanamuziki kutoka marekani Rihanna baada ya video kusamba mtandaoni akiwa anakula bata kwenye moja ya show ya baba ya mtoto wake Asap rocky. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Huddah ambaye hana uhusiano mzuri na bosi huyo wa Fenty Beuaty ameonekana kuchukizwa na hatua ya rihanna kumtekeleza mtoto wake na kwenda kujivinjari ambapo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa mastaa wengi hawajali watoo wao na ndio maana wengine wao wanapojifungua huwatelekeza watoto na kurudi  tena kwenye vilabu vya usiku. “What is the pressure on women to be outside when nursing? Isn’t the baby more important? Help me understand” Amedai. “Many have kids they don’t want just to use later as social media accessories that’s why they don’t care about their little ones…Coz chile, the way people give birth and run to the club is shocking. Have kids when ready! They will need you!” Ameongeza. Kauli yaHuddah Monore’s imekuja wiki kadhaa baada ya kuwakosoa wana mitandao maarufu wa kenya kwa hatua kusapoti bidhaa za urembo za rihanna ambazo zilizinduliwa hapa kenya huku wakisusia kutangaza bidhaa za urembo za Huddah. Rihanna pamoja na Asap Rocky walibarikiwa na mtoto mapema mwezi mei mwaka huu. Wawili hao kwa mara ya kwanza waliweka wazi taarifa njema kwa mashabiki zao kuwa wanatarajia kupata mtoto mwezi januari mwaka huu baada ya picha zao kusambaa  mtandaoni wakiwa huko Harlem Neywork city ambako Asap Rocky alizaliwa.

Read More
 HUDDAH: SIJAWAHI KUWA SINGLE MAISHANI MWANGU

HUDDAH: SIJAWAHI KUWA SINGLE MAISHANI MWANGU

Mrembo maarufu nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, Huddah Monroe anaendelea kufunguka tusioysajua kuhusu maisha yake. Kupitia instastory yake mrembo huyo amesema hajawahi kuwa single katika maisha yake yaani kwake kukaa bila mwanaume ni mwiko! “Jambo la kwanza siwezi kaa bila mwanamume, wanaume wameninunulia magari na manyumba sijawahi kuwa single maishani mwangu sijui huwa wanafanyaaje kuuwa mtu kama mimi,” amesema Huddah. Kauli yake inakuja siku chache baada ya kutusanua kwamba aliwahi kuolewa akiwa na umri wa miaka 19 na mwanamume ambaye hajamtaja jina lake. Hata hivyo, hawakupata watoto kwa sababu mwanaume wake alikuwa mraibu wa dawa za kulevya. “Nilikuwa kwenye ndoa (19), hatukuwa na mtoto na tukaachana kwa sababu mwanaume alikuwa mlevi wa dawa za kulevya! Sikuwa maarufu kwa hivyo sikuhitaji kuitangaza! So naongea kwa uzoefu. Si mzaha nyinyi nyote! Usiku mwema! Hiyo ndiyo siri yangu kubwa.” aliandika Insta Story. Utakumbuka Huddah Monroe anahusishwa kuwa na mahusiano na Staa wa Bongofleva, Jux baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja hadi kutokea kwenye video ya mwimbaji huyo, Sikuachi.

Read More
 HUDDAH MONROE AJIPIGA KIFUA KUHUSU ISHU YA KUWACHAGUA WANAUME WANAOTESHELEZA KIMAPENZI

HUDDAH MONROE AJIPIGA KIFUA KUHUSU ISHU YA KUWACHAGUA WANAUME WANAOTESHELEZA KIMAPENZI

Mrembo kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe amejisifu kuwa anajua sana kuchagua wanaume ndio maana ma-ex wake huwa wanafuatiliwa sana wanawake ambao ni rafiki zake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Huddah amesema kutokana na hilo, imekuwa ni ngumu sana kwake kwa sasa kuweka wazi mahusiano yake ila hivi karibuni anaweza kujaribu kufanya hivyo. “Kitu pekee ninchohitaji kwa mwanamume ni uaminifu na heshima, wengi wamo humu nje lakini hawana ladha, marafiki zangu wa kitambo walikuwa wanawamezea mate na kuwatafuta ma-ex wangu kwani walijua huwa nachagua vizuri”. Ameandika kupitia Instagram Ameendelea kwa kusema; “Hii ndio sababu huwa siposti mwanamume wangu mitandaoni, kwa maana wanawake watamtamani, lakini nitamposti mmoja hivi karibuni.”

Read More
 RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

RINGTONE: HUDDAH MONROE ALINITAKA KIMAPENZI NIKAMKATAA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injil nchini, Ringtone Apoko amedia kuwa mrembo maarufu mtandaoni nchini, Huddah Monroe aliwahi kumtongoza lakini akamkataa. Kauli yake inakuja mara baada ya Huddah kuibuka na kudai kuwa hajaona mwanaume ambaye amekidhi vigezo vya kuwa naye nchini Kenya. Sasa  Ringtone ameibuka na kusema “Tumekuwa na safari refu sana ya maisha na Huddah Monroe, tunajuana sana kwa vilemba, hawezi sema hivyo, umejuana miaka mingi. Ametoka mbali, labda alikuwa anatafuta kiki ama alikuwa amelewa, huwa anakunywa sana msimhukumu. Ameendelea kwa kusema,  “Hawezi sema mimi sio mtanashati na alikuwa ananililia kitambo, mimi ndio nilimkataa, alikuwa ananililia na kunisumbua sana eti ananitaka nikamkataa” “Alinitongoza nikakataa, nilimwambia lazima aokoke ndivyo tuweze tuzungumzia mambo mengine. Ni msupu. Yeye ni mmoja wa wanawake warembo zaidi barani Afrika. Hata hivyo hawezani nami kwa kuwa lazima aokoke, atubu dhambi na amkiri Yesu. Hapo ndipo tulikosania. Nilimkataa kabisa”. amesema Apoko. Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameonekana kumshangaa sana Ringtone kwa kauli yake hiyo ambayo wamedai hakuna namna ambavyo Huddah Monroe anaweza kumtaka kimapenzi ikizingatiwa kuwa hana vigezo kabisa vya kumshawishi mrembo atokee nae kimapenzi.

Read More
 HUDDAH MONROE AWACHANA VILIVYO WANAUME WANAOTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WENGI

HUDDAH MONROE AWACHANA VILIVYO WANAUME WANAOTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WENGI

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe ameamua kuwachana wanaume ambao hawawezi kutosheka na mwanamke mmoja. Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Huddah amedai kwamba hawezi kufanya mapenzi na mwanamume ambaye ana mpenzi mwingine kwani kufanya hivyo ni kujidharau. “Siwezi kufanya ngono na mwanaume ambaye ana mwanamke au mpenzi nyumbani kwake, siwezi fikiria kutoheshimika huko, wengi wenu mna nguvu kama hiyo mimi sina.” amesema. Kulingana na Huddah wanaume wengi wakiwa wadogo hawajawahi kuonyeshwa upendo wa kweli, huku hisia zao zikiumizwa. Mrembo huyo amesema wanaume wengi haswa Waafrika hawajahi pendwa vizuri wakati walipokuwa wadogo, ndio maana huwa wanalala na wanawake wengi ili kuthibitisha uwanaume wao.

Read More