Ibraah Atangaza Kuondoka Rasmi Konde Gang Baada ya Kikao na BASATA

Ibraah Atangaza Kuondoka Rasmi Konde Gang Baada ya Kikao na BASATA

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Ibrahim Abdallah maarufu kama Ibraah, ametangaza rasmi kuondoka kwenye lebo ya Konde Music Worldwide baada ya kikao cha mwisho kilichowahusisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na uongozi wa lebo hiyo. Kupitia mahojiano baada ya kikao hicho, Ibraah amethibitisha kuwa wamefikia mwafaka wa kumaliza tofauti zao na uongozi wa Konde Gang. Hata hivyo, ameeleza kuwa bado hajakabidhiwa baadhi ya vitu muhimu vinavyohusiana na kazi yake ya muziki, ikiwemo akaunti zake za digital platforms kama YouTube, Boomplay, na Spotify. Kwa upande wao, uongozi wa Konde Gang kupitia Sandra, ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa lebo hiyo, wamethibitisha kuwa Ibraah atakabidhiwa rasmi akaunti hizo kabla ya mwisho wa leo. Aidha, Sandra amemtakia kila la heri Ibraah katika safari yake mpya ya muziki nje ya Konde Gang, akisisitiza kuwa hakuna uadui kati yao bali ni mabadiliko ya kawaida katika tasnia ya sanaa. Kuondoka kwa Ibraah kunakuja baada ya muda mrefu wa tetesi na hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake ndani ya Konde Gang. Mashabiki wake sasa wanangoja kwa hamu kuona ni wapi atapeleka kipaji chake na iwapo ataendelea kung’ara kama msanii huru. Hii ni miongoni mwa migogoro ya kimikataba inayozidi kuibuka katika tasnia ya muziki Tanzania, huku mashirika kama BASATA yakihimiza mazungumzo ya kidiplomasia kama njia ya kutatua mizozo kati ya wasanii na lebo zao. Ibraah alikuwa msanii wa kwanza kusainiwa Konde Music mwaka 2020, na ametoa nyimbo kadhaa zilizotikisa chati za muziki Afrika Mashariki, kama vile One Night Stand, Nani, na Dharau akiwa chini ya lebo hiyo.

Read More
 Harmonize Ajibu Kwa Hasira Tuhuma za Kumdai Ibraah

Harmonize Ajibu Kwa Hasira Tuhuma za Kumdai Ibraah

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mwanzilishi wa lebo ya Konde Gang, Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize, hatimaye ameweka wazi uhusiano wa sasa kati yake na aliyekuwa msanii wake, Ibraah. Hili ni baada ya tetesi nyingi kuzagaa kuhusu kuvunjika kwa ushirikiano wao uliodumu kwa miaka minne. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Harmonize alithibitisha rasmi kuwa Ibraah si sehemu ya Konde Gang tena, na sasa anafanya kazi kama msanii huru. Katika kueleza hali halisi ya kuondoka kwa Ibraah, Harmonize alikanusha vikali madai kwamba alimtoza msanii huyo kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kuvunja mkataba wao. “Ni kweli mdogo wangu Chinga alinipigia simu na kuniambia anataka kutoka Konde Gang. Nilimtakia kila la kheri, lakini nikamshauri azungumze na viongozi wa lebo iwapo anahitaji kununua catalogue ya nyimbo zake,” alisema Harmonize huku akisisitiza kuwa hakuna madai yoyote ya kifedha baina yao. Harmonize aliongeza kuwa madai yaliyosambaa mitandaoni kuhusu deni hilo hayana ukweli wowote na yamekuwa yakimchafua bila sababu. “Simdai Ibraah pesa hiyo, na siwezi kupenda pesa yangu ije kunichafua mimi mwenyewe,” alisema kwa msisitizo. Katika upande mwingine wa mazungumzo hayo, Harmonize alifunguka kuhusu mustakabali wa Konde Gang, akieleza kuwa lebo hiyo iko tayari kufungua milango kwa vipaji vipya. Alisema kuwa licha ya changamoto, Konde Gang bado inaendelea na jukumu lake la kuibua na kulea wasanii chipukizi wenye ndoto kubwa. Taarifa hiyo imeibua hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, wengi wakimpongeza Harmonize kwa ukomavu wake wa kiuongozi na namna alivyosimamia suala hilo kwa hekima na utulivu. Kwa sasa, wadau wa muziki na mashabiki kwa ujumla wanasubiri kuona Ibraah atajielekeza wapi akiwa kama msanii huru, huku nafasi mpya zilizofunguliwa ndani ya Konde Gang zikisubiri kujazwa na vipaji vipya vinavyokuja na njaa ya mafanikio.

Read More
 Album ya Ibraah “The King Of New School” yafikisha streams millioni 12

Album ya Ibraah “The King Of New School” yafikisha streams millioni 12

Album ya mwimbaji kutoka Konde Gang, Ibraah “The King Of New School” iliyotoka Julai 1, mwaka huu, ikiwa pia ndio album yake ya kwanza katika safari yake ya muziki, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Milioni 12 katika majukwaa yote inapopatikana album hiyo. Hii ni habari njema kwa mashabiki wa msanii Ibraah kwani album hiyo imetumia miezi mitano pekee kupata namba hiyo kubwa. “The King Of New School” yenye jumla ya ngoma 17, Ibraah amewakutanisha wakali kama Christian Bella, Bracket, L.A.X na wengine wengi toka Afrika. Aidha, Ibraah ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki wake kwa album yake kufikisha jumla ya streams Milioni 12.

Read More
 IBRAAH AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

IBRAAH AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Ibraah ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la King of New School. Kupitia Instagram yake msanii huyo amechapisha artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 17 ya moto huku ikiwa na kolabo 6 pekee. Ibraah amewashirikisha wakali kama AY, LAX, Christian Bella, Maud Elka, Bracket, Roberto huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Usiku mwema, Maumivu, body na nyingine nyingi. Hata hivyo hajataja tarehe rasmi ya kuiachia album hiyo zaidi ya kuwataka mashabiki kuendelea kusalia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi. King of New School ni album ya kwanza kwa mtu mzima Ibraah kuitoa tangu aanze safari yake ya muziki.

Read More
 IBRAAH AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

IBRAAH AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Ibraah ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la King of New School. Kupitia Instagram yake msanii huyo amechapisha artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 17 ya moto huku ikiwa na kolabo 6 pekee. Ibraah amewashirikisha wakali kama AY, LAX, Christian Bella, Maud Elka, Bracket, Roberto huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Usiku mwema, Maumivu, body na nyingine nyingi. Hata hivyo hajataja tarehe rasmi ya kuiachia album hiyo zaidi ya kuwataka mashabiki kuendelea kusalia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi. King of New School ni album ya kwanza kwa mtu mzima Ibraah kuitoa tangu aanze safari yake ya muziki.

Read More
 IBRAAH AWEKA WAZI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

IBRAAH AWEKA WAZI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Ibraah ametangaza rasmi jina la album yake mpya ambalo ni “THE KING OF NEW SCHOOL”. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah ameweka wazi kwamba iko tayari ingawa hajataja nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake hiyo. Hii inaenda kuwa ni album ya kwanza kwa Ibraah tangu aanze safari yake ya muziki wake. Nyota huyo ambaye alitambulishwa na lebo ya Konde Music Worldwide Aprili 11, mwaka wa 2020 ameshaachia EP moja iitwayo “STEPS” yenye jumla nyimbo 5 za moto.

Read More
 IBRAAH KUFANYA VIPIMO VYA DNA KUTHIBITISHA KAMA ALIZAA NA MREMBO AITWAYE CLYNA

IBRAAH KUFANYA VIPIMO VYA DNA KUTHIBITISHA KAMA ALIZAA NA MREMBO AITWAYE CLYNA

Msanii wa bongofleva Ibraah amejibu kuhusiana na tuhuma za kumtelekeza mtoto aliyezaa na  Mrembo aitwaye Clyna aka Sugar ambaye amekuwa akijitokeza kwa mara nyingi mtandaoni tena kudai pesa ya matunzo ya mtoto wake wa kiume ambaye anadai amezaa na msanii huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah ameandika waraka mrefu huku akiambatanisha na picha ya mwanamke huyo pamoja na mtoto wake ambapo amekiri ni kweli alishawahi kuwa na ukaribu na mama wa mtoto huyo na yupo tayari kwa ajili ya vipimo (DNA) ili kuthibitisha kama kweli mtoto ni wake. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ibraa ameeleza, “Taarifa zimenifikia kwasababu mama mzazi au muhusika mkuu amenihusisha na amesema yawezekana mimi ndio mwenye bahati hii ya mtende na nimeona nipost hapa ili kuondoa dhana na maneno yanayoendelea mitandaoni au ile hofu ya kwamba pengine naweza kuwa mjinga hadi ikafikia kuitelekeza damu yangu, kitu ambacho hakiwezekani na hakitokuja wezekana. “Ni wazi kwamba mama mtoto alikuwa rafiki yangu siku za nyuma hilo halina siri na ndio maana sikusitushwa sana na hizi taarifa kama binadamu wa kawaida. Nitafata taratibu zote kwa kushirikiana na uongozi wangu pamoja na familia yangu kujihakikishia kwamba hii ni kweli damu ya Mtwara ili taratibu zingine ziendelee. Itakuwa faraja kubwa kwangu pale VIPIMO (DNA) vitakavyosema Yes huyu ni Chinga maana nitakuwa nimeshapata mwenzangu wakushirikiana nae katika safari hii ya kitendawili cha DUNIA. “Niwaahidi tu hata kama ikitokea bahati mbaya vipimo vikatoa majibu tofauti na tunayo yatarajia basi still nitakuwa rafiki bora wa malaika mtukufu ili na yeye aonje utamu wa Dunia bila masemango au kubaguliwa kwani yeye hahusiki na hajui chochote zaidi ya kuzaliwa na anategemea sisi sote tumfanye mwenye furaha” – @ibraah_tz

Read More
 IBRAAH WA KONDE GANG AKANA KUZAA MTOTO NA MWANADADA KIM MISHEPU

IBRAAH WA KONDE GANG AKANA KUZAA MTOTO NA MWANADADA KIM MISHEPU

Msanii wa Bongofleva Ibraah amekana kupata mtoto na mwanamke anayefahamika kwa jina la Kim Mishepu ambaye alitoa taarifa za kuzaa nae mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2021. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ibraah amesema taarifa hizo sio za kizushi kwa kusema kwamba ni kweli alikuwa na mototo aliyezaa na mwanamke aitwaye Pendo lakini kwa bahati mbaya alifariki akiwa na miezi mitano. Utakumbuka mwanadada Kim Mishepu aliyedai kuwa alizaa na Ibraah alimtuhumu msanii huyo kuwa amemtelekeza pamoja na motto wake baada ya kusainiwa na lebo ya konde gang inayomilikiwa na Harmonize.

Read More