Irene Ntale Atoa Kauli Tata Kuhusu Majukumu ya Kifedha kwenye Ndoa

Irene Ntale Atoa Kauli Tata Kuhusu Majukumu ya Kifedha kwenye Ndoa

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Irene Ntale, amezua mjadala mkali mtandaoni baada ya kutoa mtazamo wake kuhusu mgawanyo wa majukumu ya kifedha ndani ya ndoa. Ntale ambaye juzi kati ameingia kwenye ndoa, amesema kuwa kwenye uhusiano ulio imara na uliopangika vizuri, mwanaume anapaswa kubeba majukumu yote makubwa ya kifedha, akisisitiza kuwa hilo ni hitaji la msingi katika kuleta uongozi na utulivu ndani ya familia. Kwa mujibu wake, mwanaume ndiye anayepaswa kuhudumia gharama muhimu kama ada za shule, kodi ya nyumba, mafuta ya gari pamoja na matumizi makubwa ya nyumbani. Hitmaker huyo wa Onkubirako, ameeleza kuwa jukumu la mwanamke halipaswi kuwa mzigo wa kulipia bili kubwa, lakini akawashauri wanawake kutojiingiza katika tabia ya kudai kila kitu au kuacha majukumu madogo yakisubiri wanaume. Amesisitiza kuwa wanawake wanaweza kuchangia katika gharama ndogondogo ili kuimarisha ushirikiano wa kifamilia badala ya kuwa na mtazamo wa kutaka kusaidiwa kila jambo. Aidha, Ntale ameonya kuwa pale mwanamke anapojitwika majukumu yote ya kifedha, kuna hatari ya baadhi ya wanaume kutumia mianya hiyo vibaya.

Read More
 IRENE NTALE AWATAKA MASHABIKI WAMTAFUTIE MUME

IRENE NTALE AWATAKA MASHABIKI WAMTAFUTIE MUME

Mwanamuziki kutoka Uganda Irene Ntale hana mpenzi anayefahamika kwa muda mrefu. Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Jonathan Kyeyo, Ntale amekuwa akihangaika kutafuta mwanaume sahihi. Irene Ntale ambaye amekata tamaa sasa kwenye suala la kutafuta mume wa ndoto yake, amewapa mashabiki wake jukumu la kupendekeza mwanamume  atakayemuoa. Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Kwa kuwa nyinyi watu mnataka niolewe vibaya sana na hamwezi kuniruhusu nipumue, pendekeza mume anayefaa kwenye mitaa hii ya Twitter,” Hii si mara ya kwanza kwa Irene Ntale kupeleka matatizo yake ya mahusiano ya kimapenzi kwa mashabiki wake. Hapo awali, aliwauliza wafuasi wakekwenye mitandao ya kijamii ni kwa nini wanaume wachanga wanaogopa kumchumbia kwa ajili ya mapenzi.

Read More
 IRENE NTALE AFUNGUKA KUHUSU KUSAINIWA NA LEBO ZA MUZIKI

IRENE NTALE AFUNGUKA KUHUSU KUSAINIWA NA LEBO ZA MUZIKI

Msanii nyota kutoka Uganda Irene Ntale amesema hana mpango tena wa kujiunga na lebo yeyote ya muziki kwa ajili ya kusimamia kazi zake. Katika mahojiano yake hivi karibuni Ntale amesema ameelekeza nguvu zake kufanya muziki kama msanii wa kujitegemea kwa kuwa inalipa sana tofauti na  lebo za muziki ambazo amezitaja kuwa zinapora pesa za wasanii. Hitmaker huyo “Onkubirako” amesema hajutii kusainiwa na lebo ya muziki Universal Music Africa ikizingatiwa kuwa ilitimiza ahadi zote walizompa kwenye muziki wake. Utakumbuka Irene ntale alikuwa amesainiwa kwenye lebo ya muziki ya Swangz Avenue kabla ya kujiunga na kampuni ya Universal Music Group ambayo aliigura mwaka wa 2020.

Read More
 IRENE NTALE AKERWA NA TABIA YA VIJANA WADOGO KUMTAKA KIMAPENZI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

IRENE NTALE AKERWA NA TABIA YA VIJANA WADOGO KUMTAKA KIMAPENZI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Staa wa muziki nchini Uganda Irene Ntale amekuwa akisema kwamba yupo tayari kwa ajili ya ndoa na iwapo hilo litatimia anataka kuolewa na mwanaume wa ndoto yake. Lakini inaonekana mrembo huyo anafuatwa na vijana wadogo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene Ntale amesema hayuko tayari kuchumbiana na vijana wadogo ambapo ametoa onyo kwao kuacha tabia ya kumsumbua kwenye mitandao yake ya kijamii kama hawajafikisha umri wa miaka 30. Ikumbukwe Irene ntale amekuwa akisumbuka kumpata mwanaume atakayemuoa tangu aachane na aliyekuwa mchumba wake Jonathan Kyeyo. Jambo hilo lilimlazimu kutangaza kwamba yupo singo  na hilo limepelekea wanaume wa kila aina kuanza kumchumbia.

Read More