PALLASO AMKANA KWEUPE IVAN KARMA

PALLASO AMKANA KWEUPE IVAN KARMA

Siku chache baada ya Ivan Karma kutishia kumfungulia mashtaka Pallaso kwa kuvunja mkataba wao wa miaka mitano ghafla, msanii huyo ameamua kutia neno juu ya  tuhuma za meneja huyo wa muziki kutoka Uganda. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni msanii huyo amesema hana muda wa kuzungumzia shtuma za ivan karma kwa kuwa anatumia jina lake kutafuta umaarufu mtandaoni. Pallaso alisaini na uongozi wa Ivan Karma  mwaka wa 2019 na tangu kipindi hicho ameachia nyimbo kali ambazo zimeacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini uganda.

Read More
 PALLASO AKWEPA KESI YA KUVUNJA MKATABA NA MENEJA IVAN KARMA

PALLASO AKWEPA KESI YA KUVUNJA MKATABA NA MENEJA IVAN KARMA

Msanii Pallaso ameripotiwa kudinda kutii amri ya mahakama baaada ya meneja wake wa zamani Ivan Karma kumfungilia mashtaka kwa madai ya kukiuka mkataba wa miaka mitano wa kufanya kazi pamoja. Kulingana na wakili wa Ivan Karma, Pallaso amekuwa akikwepa kutia saini stakabadhi muhimu kwa kudai kuwa ameshikika na majukumu yake ya kikazi. Pallaso anaidaiwa kusaini mkataba unaompa Ivan Karma haki ya kuandaa shows na kutangaza kazi zake za muziki maeneo mbali mbali duniani. Jukumu la pallaso lilikuwa tu kuimba hadi pale alipoanza kufanya shows zake mwenyewe mara baada ya kutofautia kimawazo na Ivan Karma kutokana na masuala ya fedha. Mpaka sasa Pallaso ameandaa shows 90 bila uwepo wa Ivan Karma jambo ambalo limemfanya meneja wake huyo wa zamani kumtaka awajibikie shows hizo alizofanya bila idhini yake.

Read More