Pallaso anyosha maelezo kuhusu ugomvi wake na Ivien Karma.

Pallaso anyosha maelezo kuhusu ugomvi wake na Ivien Karma.

Mwanamuziki nyota nchini Uganda Pallaso amekiri kuwa hajutii kitendo cha kujiondoa kwenye uongozi wa Karma Ivien. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema hatua hiyo ya kutengana na Karma haitaathiri shughuli zake za muziki siku za mbeleni kwani meneja huyo wa muziki alimtelekeza kipindi cha korona, jambo ambalo lilimfanya kugharamia muziki wake kama msamii wa kujitegemea. Hitmaker huyo wa “Malamu” amedai kuwa baada ya msala wa Korona kuisha, aliamua kuugura uongozi wa Karma Ivien na kuendelea kujisamamia kimuziki kutokana na kitendo chake cha kusitisha kufadhili baadhi ya kazi zake. Kauli ya Pallaso imekuja mara baada ya Ivien Karma kujinasibu kuwa yeye ndiye alimkingia kifua hadi akatusua kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda ambapo alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa kuna kipindi Pallaso atakuja kujutia kuondoka kwenye usimamizi wake.

Read More
 PALLASO AKANUSHA KUTENGANA NA MENEJA WAKE IVIEN KARMA

PALLASO AKANUSHA KUTENGANA NA MENEJA WAKE IVIEN KARMA

Mwanamuziki Pallaso Mayanja amekanusha madai ya kutengana na meneja wake, Kama Ivien. Katika mahojiano, Pallaso amesema bado ana uhusiano mzuri wa kufanya kazi na Karma Ivien licha ya kutomtaja katika wimbo wake mpya “True Love”. Pallaso amesema alizidiwa na mzuka akiwa studio, hivyo akasahau kumpa shavu meneja wake. “Nitakapoacha kufanya naye kazi, nitaweka wazi kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii. Bila tamko rasmi kutoka kwangu, usiamini uvumi huo,” Pallaso amebainisha. Ikumbukwe mapema wiki iliyopita ripoti zilidai kuwa wawili hao waliingia kwenye ugomvi kutokana na masuala yanayofungamana na pesa.

Read More