Tems, Doja Cat na J Balvin Kuwasha Jukwaa la Club World Cup Usiku Huu

Tems, Doja Cat na J Balvin Kuwasha Jukwaa la Club World Cup Usiku Huu

Usiku wa leo, majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, macho na masikio ya mashabiki wa soka duniani yatakuwa yameelekezwa kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani, ambako fainali ya FIFA Club World Cup itapigwa kati ya mabingwa wa Ulaya, Chelsea FC kutoka England, na mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG). Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na wa kiwango cha juu, ukiwa ndio hitimisho la mashindano hayo ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu. Katika kilele cha tukio hilo, kutakuwa na Halftime Show ya aina yake, ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano ya Club World Cup, kutafanyika onesho la burudani kipindi cha mapumziko. Wasanii watatu wakubwa duniani, Doja Cat kutoka Marekani, J Balvin kutoka Colombia, na Tems kutoka Nigeria watatumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya uwanja na wale wanaotazama kupitia runinga duniani kote. Tukio hili la kihistoria linaashiria hatua mpya katika kuunganisha michezo na burudani, na linathibitisha hadhi ya soka kama jukwaa pana la utamaduni wa dunia.

Read More