Jackie Chandiru: Sitoweka Tena Mahusiano Yangu Mtandaoni
Msanii kutoka Uganda, Jackie Chandiru, amesema kuwa amejifunza kutokana na changamoto za mahusiano aliyopitia hapo awali, na hatoweka tena maisha yake ya kimapenzi hadharani. Akizungumza kuhusu safari yake ya mapenzi, Chandiru ambaye aliwahi kung’ara kama mwanachama wa kundi la Blu 3, amesema kuwa zamani alikuwa akionesha wazi wapenzi wake kwenye mitandao ya kijamii, hatua ambayo ilimletea madhara baada ya wasichana wa Kampala kuvunja mahusiano yake. Hitmaker huyo wa Gold digger, meelezea kuwa sasa anaamini kwa uthabiti kuwa kuweka uhusiano faraghani ni uamuzi mzuri zaidi kwa manufaa ya mahusiano hayo. Chandiru amethibitisha kuwa kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini amesisitiza kuwa hatawahi kuomuonesha mpenzi wake mtandaoni kwa sababu anataka kumlinda dhidi ya usumbufu wa umma. Aidha, ameongeza kuwa kuweka picha au video za wapenzi mitandaoni si kipimo cha mapenzi, bali mara nyingi ni njia ya kutafuta umaarufu wa haraka.
Read More