Jackie Matubia: Sihusiki na Sakata la Ellah na Odek

Jackie Matubia: Sihusiki na Sakata la Ellah na Odek

Mwigizaji na mama wa watoto wawili, Jackie Matubia, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya jina lake kuhusishwa na drama ya kifamilia inayomkumba Ellah Ray, dada yake sosholaiti Amber Ray, na aliyekuwa mchumba wake Steve Odek. Matubia, amesema hana uhusiano wowote na sakata hilo na ameonya watu wanaomchafulia jina kutumia uvumi mitandaoni. Kupitia Insta Story yake, alikanusha madai hayo akieleza kuwa amechoshwa na tabia ya watu kutumia akaunti feki kumhusisha na kashfa ambazo hazina msingi. Mrembo hyo alisisitiza kuwa, iwapo watu wanataka kumuhusisha na mambo ya uhusiano, basi angalau wawe na ushahidi wa kweli, kwani kwa sasa wanamtupia lawama zisizomhusu. Kauli yake imeweka bayana msimamo wake wa kutoshirikiana na sakata hilo na kutaka jina lake libaki safi. Jackie alilazimika kujibu baada ya Ellah Ray kumuanika Steve Odek kwa usaliti na kudai anahusiana na wanawake kadhaa, jina la Matubia likiwemo katika tetesi hizo.

Read More
 Jackie Matubia Akanusha Madai ya Kuvunja Ndoa ya Mtu

Jackie Matubia Akanusha Madai ya Kuvunja Ndoa ya Mtu

Mwigizaji wa Kenya, Jackie Matubia, hatimaye amevunja ukimya wake kufuatia madai mazito yaliyomhusisha na kuvunjika kwa ndoa ya mwanamke mmoja. Akizungumza baada ya sakata hilo kusambaa mitandaoni, Matubia amekanusha madai hayo, akisema hayana msingi wowote. Ameeleza kuwa taarifa hizo zilibuniwa kwa lengo la kumchafua na kumharibia jina mbele ya mashabiki wake na umma kwa ujumla. Mrembo huyo amesema kwamba kama kweli angekuwa amenunuliwa gari na nyumba na mume wa mwanamke huyo, asingekuwa katika hali ya kuhangaika kila siku kutafuta kipato cha kuendesha maisha yake. Hata hivyo, Matubia amewataka Wakenya kutoamini taarifa hizo, akisisitiza kuwa zinaenezwa kwa nia ya kumvunjia heshima. Wiki hii, mwanamke mmoja kupitia Instagram Stories za bloga Edgar Obare, alimtuhumu Matubia kwa kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake. Mwanamke huyo alidai kuwa wakati Matubia akiigiza kwenye kipindi cha Zora, alihusiana kimapenzi na mume wake, ambaye pia alinaswa akihusishwa na Shirika la Ujasusi (NIS). Hata hivyo, Matubia amewataka Wakenya kutoamini taarifa hizo, akisisitiza kuwa zinaenezwa kwa nia ya kumvunjia heshima. Tukio hili limeendelea kuzua gumzo mitandaoni huku mashabiki wakisubiri kuona hatua atakazochukua dhidi ya madai hayo.

Read More
 Jackie Matubia Aeleza Changamoto Alizopitia Katika Malezi ya Pamoja na Ex Wake

Jackie Matubia Aeleza Changamoto Alizopitia Katika Malezi ya Pamoja na Ex Wake

Muigizaji maarufu wa Kenya, Jackie Matubia, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizokumbana nazo alipokuwa akijaribu kulea mtoto kwa ushirikiano (co-parenting) na aliyekuwa mpenzi wake, Blessing Lung’aho. Akiwa mgeni kwenye G2G Podcast, Jackie alisema alijitahidi kwa dhati kuhakikisha kuwa mtoto wao analelewa katika mazingira ya upendo na ushirikiano, lakini juhudi zake hazikueleweka vyema na Lung’aho. “Nilijaribu, marafiki zake waliona. Nilikuwa namsogelea alipokuwa, hata kumtembelea, lakini alidhani nataka turudiane,” Jackie alieleza kwa hisia. Matubia alibainisha kuwa nia yake kuu ilikuwa kumpa mtoto wao nafasi ya kuwa karibu na wazazi wote wawili, licha ya uhusiano wao wa kimapenzi kuvunjika. Alisema kuwa alifanya jitihada nyingi kuhakikisha Blessing anahusishwa katika malezi, lakini mambo hayakuenda kama alivyotarajia. Hii ni mara ya kwanza kwa Jackie kuzungumza kwa uwazi kuhusu hali ya mahusiano yao baada ya kuachana, na kauli yake imeibua hisia mbalimbali miongoni mwa mashabiki wake na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wengi wamemsifia kwa ujasiri wa kuweka mbele maslahi ya mtoto wake licha ya changamoto za kibinafsi. Jackie Matubia na Blessing Lung’aho walikuwa wapenzi maarufu kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutengana mwaka jana. Wawili hao walibarikiwa na mtoto mmoja katika kipindi cha uhusiano wao.

Read More