Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Mchekeshaji aliyegeùkia siasa Jalang’o amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mke wa Bahati, Diana B. Kwenye mahojiano na Mungai Eve, Jalango ambaye ni mbunge wa Lang’ata amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na Diana ulikuwa ni wa kirafiki tu. Aidha amenyosha maelezo kuhusu picha inayosambaa mtandaoni akiwa na Diana kwa kusema kuwa alipiga picha hiyo na mama huyo wa watoto watatu takriban miaka 15 iliyopita alipokutana naye kwenye duka moja la jumla jijini Nairobi. “I remember that photo must have been taken in 10-15 years old at Jamia mall. She requested for a photo and I took a photo with her. I have never dated Diana. Diana has been my friend for the longest time and even when we took that photo it was just a good photo.”, Alisema. Kauli yake imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa wawili hao walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma kutokana na hatua ya Diana B kukiri hadharani kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume matajiri kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.

Read More
 JALANG’O AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA KUTOKEA KWENYE VILABU VYA BURUDANI

JALANG’O AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA KUTOKEA KWENYE VILABU VYA BURUDANI

Mtangazaji wa radio ambaye kwa sasa ni mbunge mteule wa Lang’at Felix Oduor maarufu Jalang’o amedokeza mpango kufanya kipindi cha asubuhi kwenye radio. Katika kikao cha maswali na majibu kwenye Instagram Jalang’o amesema ana upendo kwa radio kwa kuwa ni chombo ambacho kimemfungulia milango nyingi katika maisha yake. Hata hivyo mwanasiasa huyo amesema hatakuwa mshereheshaji kwenye maonyesho ya burudani  lakini pia hatatokea kwenye vilabu vya burudani kutokana na majukumu mengi ambayo yatakuwa yanamuandama kama mbunge wa Lang’at. Utakumbuka jalango alimbwaga  mbunge wa langat anayeondoka Nixon Korir wa UDA kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika majuzi nchini Kenya.

Read More
 PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

PREZZO, SANAIPEI TANDE NA JALANG’O KUSHIRIKI SHOW MPYA YA UCHESHI IITWAYO ROAST HOUSE

Rapper Prezzo, Sanaipei tande na Mchekeshaji maarufu nchini ambaye pia ni mgombea wa ubunge langat  Jalang’o wametajwa kuwa miongoni mwa mastaa 10 na wachekeshaji 17 wa kenya  ambao watarajiwa kushirikishwa  kwenye show mpya ya ucheshi iitwayo Roast House. Show hiyo inalenga kusherekea mafanikio na machango wa mastaa mbali mbali nchini Kenya kupitia ucheshi ambao utafanywa na kundi la wachekeshaji wa majukwaani. Roast House ina maonyesho au Episodes 10 za dakika 24 kila moja ambayo itawapa nafasi kwa wachekeshaji kutoa burudani na vichekesho wakiangazia madai, kauli mbiu na matukio mbali mbali maishani kwa ajili mastaa watakao kuwa wamealikwa. Roast House ambayo itaruka hewani Julai 14 mwaka huu imetayarishwa na eugene mbugua kwa ushirikiano na D & R studios pamoja na makundi ya wachekeshaji kutoka nchini Kenya.

Read More
 NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

NADIA MUKAMI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJA UZITO WAKE NA ARROW BOY

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ameshindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni kuhusu uja uzito wake na Arrow boy. Kupitia video aliyoishare kwenye ukurasa wake wa instagram Nadia Mukami amedokeza kuwa alipoteza uja uzito wake mwishoni mwa mwaka wa 2021. Hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” amesema licha ya kupoteza uja uzito wake aliahuma kutoweka wazi habari hiyo mbaya kwa umma. Hata hivyo amemtolea uvivu Jalang’o kwa  madai ya kusema kuwa hataomba msamaha kwa hatua ya kuanika uja uzito wake akiwa redioni akisema kwamba kitendo hicho sio cha kingwana.. Kauli ya Nadia Mukami imekuja mara baada ya Jalang’o kutangaza redio kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mchumba wake Arrow Boy hivi karibuni. Jambo ambalo lilimkasirisha Arrow Boy ambapo alitumia instastory kumuonya Jalang’o akome kuingilia maisha yake na nadia mukami. Kutokana na hilo Jalang’o alimjibu Arrow Boy kwa kusema kwamba atakoma kuzungumzia maisha yao na hajutii kuweka wazi uja uzito wa Nadia Mukami.

Read More
 ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

Staa wa muziki nchini Arrow Boy kwa mara nyingine amekanusha tetesi za mchumba wake Nadia Mukami kuwa na uja uzito wake. Hii ni baada ya mchekeshaji Jalang’o kwenye kipindi cha Jalas and Kamene in the morning kinachoruka kupitia Kiss 100 kusisitiza kuwa Nadia Mukami ni mjamzito na alithibitisha hilo wakati wapenzi wawili hao walimtembelea kijiji kwao. Jalango alienda mbali zaidi na kumshauri Nadia Mukami aache ishu ya kuficha uja uzito kwa umma kwani hivi karibuni itajulikana tu. Sasa akijibu hilo Arrow Boy kupitia instastory ameandika ujumbe unaosomeka “2022 Wanaume Tupunguze Mshene Bana biashara Haikuhusu achana nayo Kabisa shugulika na maisha yako” ujumbe ambao umetafsiri kumlenga moja kwa moja Jalang’o. Juzi kati Nadia Mukami aliripotiwa kuwa na uja uzito wa Arrow Boy hii ni baada ya kuonekana akitumbuiza kwenye show moja akiwa amevalia mavazi makubwa jambo ambalo liliwafanya wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ni mjamzito. Hata hivyo Nadia Mukami kupitia Instagram page yake amenyosha maelezo kwa kupost picha ambayo imezima kabisa tetesi za kuwa na uja uzito.

Read More