Msanii wa Injili Janet Otieno Awabariki Mashabiki na EP Mpya

Msanii wa Injili Janet Otieno Awabariki Mashabiki na EP Mpya

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Janet Otieno ameanza msimu mpya wa huduma yake ya muziki kwa kuachia rasmi EP yake ya kwanza iitwayo “Unaposhuka”, ambayo sasa inapatikana katika majukwaa yote ya muziki mtandaoni. Kupitia ujumbe wake kwa mashabiki, Janet ameeleza kuwa amefurahia sana kuachia kazi hii mpya ambayo imebeba ujumbe wa kumtukuza Mungu. Msanii huyo amesema EP hiyo imebeba jumla nyimbo sita za moto na ina nyimbo kama Jina Lako, Unaposhuka, Unastahili, Mwamba Imara, Salama na Mwaminifu. Hata hivyo amesema kuwa hii ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki wa injili na ni mwanzo wa msimu mpya wa kuinua mioyo ya mashabiki zake kupitia nyimbo zenye mafunzo na faraja. Kwa sasa, Unaposhuka EP inapatikana kwenye majukwaa yote ya kusikiliza muziki ikiwemo Spotify, Boomplay, YouTube na Apple Music

Read More
 JANET OTIENO KUTOA MSAADA KWA FAMILIA ZENYE UHITAJI, TURKANA

JANET OTIENO KUTOA MSAADA KWA FAMILIA ZENYE UHITAJI, TURKANA

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Janet Otieno amezindua kampeni yake ambayo inalenga kutoa msaada kwa wakaazi wa kaunti zilizoathrika na ukame Kaskazini mwa Kenya. Katika mahojiano na Mungai Eve Bi. Otieno ameeleza nia ya kufanya hivyo ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na mchango mkubwa alioupata kupitia muziki wake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Napokea kwako” amedokeza kuwa ataanza kampeini hiyo katika kaunti ya turkana kabla kueleka kaunti zingine zilizoathirika na ukame ambapo amesema anapanga kutoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine ya msingi kwa familia zenye uhitaji kaunti hiyo akishirikiana na washirika wengine wa maendeleo. Sanjari na hilo Mwanama huyo ameweka wazi matamanio yake ya kuingia kwenye siasa kwa kusema kwamba muda sahihi ukifika ataweza wazi azma yake ya kuwa mwanasiasa ila kwa sasa anaendelea na huduma ya kueneza injili kupitia nyimbo zake. Utakumbuka Janet Otieno amerejea nchini majuzi akitokea nchini Marekani ambako amekuwa kwenye ziara yake ya kimuziki aliyoipa  jina la “Napokea kwako.”

Read More