JASON DERULO ATAJA SABABU YA MASHINDANO YA MUZIKI KUFELI KUTOA MASTAA

JASON DERULO ATAJA SABABU YA MASHINDANO YA MUZIKI KUFELI KUTOA MASTAA

Msanii nyota kutoka nchini Marekani Jason Derulo amefunguka sababu zinazofanya mashindano mengi ya uimbaji kushindwa kutoa Mastaa wenye uwezo wa kiushindani wanapoingia kwenye muziki. Kwenye mahojiano na Billboard, Jason amesema mashindano mengi kama The Voice Chilevision na American Idol hushindwa kutoa Mastaa kwa sababu huzingatia sauti ya msanii pekee na kusahau vitu vya ziada. Msanii huyo amemtolea mfano msanii Cardi B kuwa alipata umaarufu kabla hata ya kuanza kuimba kwa sababu alikuwa na vitu vya ziada. “I think a lot of times in these competition-based shows, they’re not looking for a special thing about a person but they’re looking for the best voice. Unfortunately, that is not what makes a star. It’s a special something about somebody that makes a star,” Amesema Jason. Ameongeza “Cardi B, before she put out any music, people were into Cardi B, she had that special something,”

Read More
 JASON DERULO AMPIGA MTU NGUMI YA USO KISA KUITWA USHER

JASON DERULO AMPIGA MTU NGUMI YA USO KISA KUITWA USHER

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jason Derulo anadaiwa kuwashambulia watu wawili baada ya watu hao kumwita jina la “Usher” Kwa mujibu wa TMZ wameripoti kuwa tukio hilo limetokea kwenye Hoteli moja huko Las Vegas nchini Marekani. Mashahidi wanasema kuwa mtu mmoja alimwita Jason kwa jina la Usher jambo ambalo lilimchukiza staa huyo na kuanza kumshambulia kwa kumpiga ngumi ya uso mtu huyo kisha kuhamia kwa mtu mwingine na kumshambulia pia. Mpaka sasa watu hao hawajafungua mashitaka yoyote dhidi ya staa huyo lakini inawezekana huko mbeleni wakafungua mashtaka endapo wakibadili mawazo yao. Pamoja na kujeruhiwa huko watu hao hawajaenda hospitali yoyote kupata hata huduma ya kwanza

Read More