Jay Melody Amtishia Mtu Aliyemvunjia Heshima: Siku Moja Utaishia Jela!”
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody, ameacha mashabiki wake wakibaki na maswali baada ya kuandika ujumbe wa mafumbo kwenye Insta Story yake, hatua iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni. Katika ujumbe huo, Jay Melody ameandika kwa mtindo wa onyo akimtahadharisha mtu ambaye hakumtaja moja kwa moja kwamba endapo ataendelea na tabia zake za usela anaweza kujikuta matatani na hata jela. Hitmaker huyo wa Mtoto ameongeza kuwa mtu huyo mara kwa mara huonekana akileta miyeyusho na kushindwa kuaminika, hali inayomfanya aonekane kama chizi machoni pa watu. Jay Melody pia amesisitiza kwamba siku moja mtu huyo ataingia katika matatizo makubwa na kuishia kujuta kwa matendo yake. Ujumbe huo uliachwa bila maelezo zaidi, jambo lililoacha mashabiki wake wakijiuliza kama msanii huyo alikuwa anamwandikia mtu maalum au alikuwa akizungumza kwa ujumla kuhusu maisha na tabia za baadhi ya watu. Mashabiki kadhaa mitandaoni wameonyesha hisia tofauti, wengine wakichukulia kama ujumbe wa mafundisho, huku wengine wakihisi huenda ni dongo lililotumwa kwa mtu maarufu.
Read More