Jeezy Adai Jay Z Alimtoa Kwenye Wimbo wa Beyoncé

Jeezy Adai Jay Z Alimtoa Kwenye Wimbo wa Beyoncé

Rapa kutoka Marekani, Jeezy, amefunguka kuhusu tukio lililomkuta nyuma ya pazia la utengenezaji wa wimbo maarufu wa Beyoncé “Drunk In Love”. Jeezy ameeleza kuwa awali alikuwa sehemu ya mradi huo, tayari akiwa ameandika verse yake kwa ajili ya kushiriki kwenye wimbo huo, lakini mambo yalibadilika ghafla. Kwa mujibu wa Jeezy, baada ya maandalizi ya awali kukamilika, alipokea taarifa kutoka kwa Jay Z akielezwa kuwa hatakuwa tena kwenye wimbo huo, na kwamba Jay Z mwenyewe ndiye atakayeshirikiana na Beyoncé kwenye ngoma hiyo. Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mtandaoni huku mashabiki na wachambuzi wa muziki wakigawanyika. Wapo wanaodai huenda verse ya Jeezy haikuwa na mvuto wa kutosha, jambo lililomfanya Jay Z kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, wengine wanaamini verse ya Jeezy ilikuwa kali kupita kiasi, hali iliyoweza kumfanya Jay Z kuhofia Jeezy angefika mbali zaidi kupitia wimbo huo. Aidha, baadhi ya wapenzi wa muziki wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa verse ya Jay Z kwenye Drunk In Love haikuwa kali sana, na huenda ingekuwa busara zaidi kumuacha Jeezy ashiriki.

Read More
 Nicki Minaj Afunguka Kuhusu Sakata la Deni la Tidal

Nicki Minaj Afunguka Kuhusu Sakata la Deni la Tidal

Mwanamuziki maarufu wa hip hop, Nicki Minaj, ameibua shinikizo kwa rapa na mwekezaji, Jay-Z, akidai kuwa anamdai kati ya dola milioni 100 hadi 200 baada ya kuuza mtandao wa kusikiliza muziki wa TIDAL mwaka 2021. Katika madai haya ambayo yamezua gumzo mitandaoni, Nicki amesema kuwa alikuwa mmoja wa wasanii wa awali kumiliki sehemu ya mtandao huo na alifanya juhudi kubwa zaidi za kuitangaza TIDAL, ikiwemo kuliko msanii mwenzake, Beyoncé, wakati wa uzinduzi wa mtandao huo. “Nilipambana sana kutangaza TIDAL, zaidi hata ya Beyoncé,” alisema Nicki. Nicki anadai kuwa wakati Jay-Z aliuza mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square, inayomilikiwa na Jack Dorsey aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, kwa kiasi cha dola milioni 300, wasanii wenzake walilipwa kati ya dola milioni 8 hadi 9 kila mmoja, lakini yeye hakuambulia hata senti. Zaidi ya hayo, Nicki amesema alipokea ofa ya dola milioni 1 (takriban Shilingi bilioni 2.6) ili kutuliza madai haya, lakini alikataa. “Nilipewa ofa ya dola milioni moja ili ninyamaze, lakini sikuikubali. Mashabiki wangu wanastahili kujua ukweli,” alisema Nicki. Madai haya yamepokelewa kwa msisimko mkubwa, huku mashabiki wake, maarufu kama Barbz, wakimpongeza kwa kuonyesha maadili ya kuhimiza uwazi na haki, hasa kwa kuwa Nicki alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya TIDAL kuwa mtandao maarufu. Kwa historia, Jay-Z alinunua TIDAL mwaka 2015 kwa dola milioni 56 na baadaye kuuza hisa nyingi za mtandao huo kwa kampuni ya Square kwa dola milioni 297 (kama Shilingi bilioni 689+). Wasanii wengine wamiliki wa mtandao huo ni pamoja na Alicia Keys, Beyoncé, J. Cole, Kanye West, Lil Wayne, Rihanna, T.I, pamoja na Nicki Minaj mwenyewe. Madai haya yanazua mjadala mzito katika tasnia ya muziki na uwekezaji, huku wengi wakisubiri maelezo rasmi kutoka kwa Jay-Z na kampuni ya Square kuhusu madai ya Nicki Minaj.

Read More
 Jay-Z na Jonathan Mannion wamaliza tofauti zao nje ya mahakama

Jay-Z na Jonathan Mannion wamaliza tofauti zao nje ya mahakama

Jay-Z ameafikiana na Jonathan Mannion kwenye shtaka ambalo Rapa huyo mkongwe na Mfanyabiashara alimshtaki mpiga picha huyo ambaye alikuwa nyuma ya cover za Album kama ‘Reasonable Doubt, ‘Hard Knock Life’ na The Blueprint. Hov alimshtaki Mannion na Kampuni yake mwezi June 2021 kwa madai ya mpiga picha huyo kunufaika kupitia Jina lake kwa kuuza picha zake kwenye tovuti pasina ridhaa. Malalamiko hayo yalidai Mannion amekuwa akitengeneza Maelfu ya Dola za Kimarekani. Baada ya Jay-Z na Roc Nation kumpiga marufuku, Mannion alidaiwa kutaka kitita kirefu cha pesa. Shtaka hilo lilitajwa kuanza kuunguruma Mahakamani mwezi March mwaka huu, lakini Jay-Z na Jonathan Mannion wanaonekana kuwa tayari wameyamaliza nje ya Mahakama hivyo shtaka hilo halitofika tena Mahakamani. Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama zilizodakwa na mtandao wa AllHipHop, Jay-Z na Jonathan Mannion wamemuomba Jaji kuiondoa kesi hiyo Mahakamani wakieleza kwamba wamekubaliana kumalizana. Mahakama imewataka kuwasilisha hati za makubaliano yao hadi Februari 17 mwaka huu.

Read More
 Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Rapa 50 Cent hakubaliani na hoja isemayo kwamba Jay-Z ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hip Hop kuliko Eminem. 50 Cent ameipinga hoja hiyo ambayo imesemwa na nyota wa zamani wa NBA, Jamal Crawford kwenye podcast ya Shaquille O’Neal, 50 Cent alishuka kwenye comment na kusema ni upuuzi mtupu. Sio mara ya kwanza kwa 50 Cent kumkingia kifua Eminem hasa pale inapokuja mijadala mizito ya muziki wa Hiphop, itakumbukwa Oktoba 2022 kwenye mahojiano na Ebro in The Morning, 50 Cent alisema “Rap God” Eminem hapewi heshima ambayo anastahili.

Read More
 Jay Z kusaidia kukamilisha onesho la Rihanna kwenye Super Bowl

Jay Z kusaidia kukamilisha onesho la Rihanna kwenye Super Bowl

Rapa kutoka Marekani Jay-Z ametajwa kuhusika kwenye mpangilio wote wa onesho la Rihanna kwenye Halftime show ya Super Bowl ambayo itafanyika Februari 12, mwaka 2023. Jay-Z ambaye alimsaini Riri kwenye label ya Def Jam mwaka 2005, alianza kuihudumia NFL kwenye sekta ya burudani tangu mwaka 2019 ambapo kwenye utawala wake alifanikiwa kuangusha performance kubwa ya Kihistoria mwaka 2022 kwa kuwaleta pamoja, Dr. Dre, Mary J. Blidge, Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem na 50 Cent.

Read More
 Baba mzazi wa Rapa Tory Lanez amshtumu Jay Z kwa kuhujumu kesi inayomkabili mwanaye

Baba mzazi wa Rapa Tory Lanez amshtumu Jay Z kwa kuhujumu kesi inayomkabili mwanaye

Baba mzazi wa Rapa Tory Lanez ameonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama kumkuta na hatia mwanaye kwenye shtaka la kumpiga risasi Megan Thee Stallion ambapo huenda akahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 20 gerezani. Akiwa nje ya Mahakama, mzee huyo Sonstar Peterson, amemshtumu rapa Jay-Z pamoja Roc Nation kuwa wamehusika nyuma ya pazia kwenye maamuzi hayo. Familia nzima ya Tory Lanez imeonesha kuwa na hasira na Jay-Z pamoja na Beyonce wakidai kufanyiwa mchezo mchafu na familia hiyo. Jay-Z anatajwa kuhusika hadi kwenye kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo. Ikumbukwe mwezi Juni mwaka 2022, Jay-Z alitangaza kumsaini Megan Thee Stallion ndani ya Roc Nation.

Read More
 JOE BUDDEN AANIKA MADHAIFU YA JAY Z KWA UMMA

JOE BUDDEN AANIKA MADHAIFU YA JAY Z KWA UMMA

Rappa na Mtangazaji kutoka nchini Marekani Joe Budden hajaona sababu yoyote ya kuikalia kimya kauli ya rappa Jay Z kuto toza kiasi chochote cha pesa katika ngoma anazo shirikishwa. Akiwa kwenye Episode mpya ya Flip Da Script podcast, Budden amesema Jay Z aliwahi kumtoza kiasi cha $250k ili kumpata kwenye remix ya ngoma yake ya “Pump It Up” Utakumbuka hivi katibuni Jigga alifanya mahojiano na Mchekeshaji Kevin Hart kupitia podcast ya “Hart to Heart” ambapo alifunguka kuto toza kiasi chochote cha pesa katika nyimbo anazoshirikishwa.

Read More
 JAY Z AFUNGUKA SABABU ZA KUTOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

JAY Z AFUNGUKA SABABU ZA KUTOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

Rapa kutoka Marekani Jay-Z anazidi kutufunulia kurasa za kitabu cha maisha yake kwa kufunguka mengi kuhusu yeye, na sasa ni kurasa ya mitandao ya kijamii. Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na mchekeshaji kevin Hart kupitia podcast ya “Hart to Heart”,Jay-z amefunguka sababu zinazomfanya kutotumia mitandao ya kijamii kwa kile anachodai kuwa mitandao hiyo sio kwaajili yake na sio sehemu ya yeye kujihusisha japo anaamini katika Mageuzi. “It’s not for me. It’s not for me to engage. I didn’t grow up in that space,” “I believe in evolution so whatever form it is, I accept that”. Amesema Jay Z. Utakumbuka Jigga anahistoria ya kuingia mara mbili katika mtandao wa Instagram, Mwaka 2015 alijiunga katika mtandao huo kutoa heshima zake katika kumbukizi ya miaka 57 ya kuzaliwa kwa Marehemu Michael Jackson na 2021 alijiunga tena kuitangaza filamu ya The Harder They Fall.

Read More
 JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

Orodha ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza pesa nyingi zaidi mwaka wa 2021 imetoka na jina la Jay-Z lipo namba 1. Jay Z ametajwa kuingiza kiasi cha shilling billion 51.2 za Kenya  ambazo zimetokana na pato la baada ya kuuza hisa zake nyingi za mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square Ink, kwa takriban shilling billion kiasi cha shilling billion 34.4 za Kenya. Lakini pia Jay Z alikunja mkwanja mrefu mwaka jana baada ya kampuni ya LVMH kununua nusu ya hisa za Kinywaji chake, cha Armand de Brinac. Kwa upande wa Kanye west ambaye amekamata nafasi ya pili kwa shilling billion 28.5 za Kenya, pato lake kubwa limeendelea kuingia kupitia bidhaa za Yeezy. Wasanii wengine waliongiza pesa nyingi mwaka wa 2022 ni pamoja na Diddy ambaye alikamata nafasi ya tatu kwa shilling billion 8.5 akifuatwa na drake aliyeingiza kiasi cha shilling billion 5.7 huku tano bora ikifungwa na mtu mzima wiz khalifa ambaye aliingiza kiasi cha shilllingi billion 5.1 za Kenya. HIP-HOP’S TOP EARNERS 2021 JAY-Z – $470 million Kanye West – $250 million Diddy – $75 million Drake – $50 million Wiz Khalifa – $45 million Travis Scott – $38 million DJ Khaled – $35 million Eminem – $28 million J. Cole – $27 million Birdman – $25 million Doja Cat – $25 million Tech N9ne – $25 million

Read More
 KUMBE THE GAME ALIMTUPIA JAY Z MATUSI MAZITO BAADA YA KUMNYIMA NAFASI YA KUTUMBUIZA KWENYE SUPER BOWL 2022

KUMBE THE GAME ALIMTUPIA JAY Z MATUSI MAZITO BAADA YA KUMNYIMA NAFASI YA KUTUMBUIZA KWENYE SUPER BOWL 2022

Rapa The Game kutoka Marekani amekasirika sana baada ya kukosa nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022, Wiki iliyopita alitokwa mapovu na kusema 50 Cent hakustahili kupewa nafasi hiyo. Meneja wake aitwaye Wack 100 ameibuka na kutusanua makubwa ambayo hatuyafahamu nyuma ya pazia. Wack 100 amesema The Game alimtukana Jay-Z tusi zito “Suck My D**k” baada ya kumnyima nafasi ya kutumbuiza kwenye Halftime show ya fainali hizo za mwaka huu. Utakumbuka Roc Nation ya Jay Z waliingia makubaliano na NFL kuwa waandaaji wa burudani kwenye Super Bowl 2022. Kinyongo baina ya wasanii hao kilianza mwaka 2005 baada ya The Game kudai kwamba alijibiwa vibaya na Jay-Z walipokutana kwenye mgahawa wa 40/40 mjini New York ambapo The Game alimuomba ushauri Jigga ya namna ya kudumu muda mrefu kwenye muziki.

Read More
 JAY Z KUMFUNGULIA MASHTAKA MPIGA PICHA WAKE KWA KUTUMIA PICHA ZAKE BILA IDHINI

JAY Z KUMFUNGULIA MASHTAKA MPIGA PICHA WAKE KWA KUTUMIA PICHA ZAKE BILA IDHINI

Rapa mkongwe kutoka Marekani Jay-Z ameamua kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpiga picha wake kwa madai ya kutumia picha zake Kibiashara bila idhini yake. Baada ya kushindwa kufikia makubaliano nje ya mahakama, sasa shtaka hilo limetajwa kuwa litaanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu. Mwaka jana Jay-Z alifungua mashtaka akidai kwamba mpiga picha huyo aitwaye Jonathan Mannion ambaye alihusika kupiga picha zilizotumika kwenye album cover ya ‘Reasonable Doubt’ alichukua picha zilizobaki na kuziuza kwenye tovuti yake bila idhini.

Read More
 JAY Z AJINASIBU HAKUNA WAKUSHINDANA NAYE KWENYE VERZUZ

JAY Z AJINASIBU HAKUNA WAKUSHINDANA NAYE KWENYE VERZUZ

Rapa mkongwe kutoka nchini Marekani Jay Z amefunguka kuhusu VERZUZ na kujigamba kwamba hakuna msanii yeyote ambaye anaweza kusimama na kushindana naye kwenye Jukwaa hilo. Kupitia Twitter Spaces ambayo iliwakutanisha pamoja na Alicia Keys na wadau wengine wa muziki kujadili kuhusu album mpya ya Alicia Keys ‘KEYS’ Jay-Z alisikika akisema “Hakuna wa kusimama/kushindana na mimi kwenye Jukwaa la Verzuz. Siwezi kudanganya, na wala simkosei mtu yeyote heshima. Kila mmoja ni mkali, wamefanya kile walichofanya. Hakuna wakusimama na mimi kwenye ile steji. Hakuna nafasi hiyo kamwe kwamba mtu yeyote kusimama na mimi kwa muda wa masaa mawili, haiwezi kutokea kamwe.” alifunguka na kupigilia msumari pia kwamba hatokuja kushiriki Verzuz. Hivi karibuni rapa Rick Ross alitangaza uwezekano wa kusimama na Jay-Z na kushindana naye kwenye Jukwaa la Verzuz.

Read More