Rahmah Pinky afunguka chanzo cha kuondoka Team No Sleep

Rahmah Pinky afunguka chanzo cha kuondoka Team No Sleep

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Uganda Rahmah Pinky amevunja kimya chake juu ya kutengana na meneja wa vipaji, Jeff Kiwa. Pinky ameelezea kuwa Jeff Kiwa alipoteza mweelekeo kwenye suala la kusimamia muziki wake na akaanza kumtaka kimapenzi, jambo ambalo anadai hakuweza kulivumilia. “Mawazo yake yalibadilika na akaanza kutaka mambo mengine kutoka kwangu, ilibidi niikimbie lebo yake ya TNS kwa sababu sikutaka kukubali njia aliyotaka niifuate,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Kauli ya Pinky imekuja mara ya kudaiwa kuwa alitimuliwa kwenye lebo TNS inayoongozwa na Jeff Kiwa kwa kukosa nidhamu. Inaidaiwa kuwa licha ya kuonywa mara kwa mara kubadili mienendo yake, alipuuza ushauri wa uongozi wake na kuendelea kuvuta shisha huku akitoka kimapenzi na wanaume tofauti kwenye nyumba ambayo lebo ilimkodishia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake za kisanaa.

Read More
 SHEEBAH KARUNGI AFUTA UTAMBULISHO WA TEAM NO SLEEP KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

SHEEBAH KARUNGI AFUTA UTAMBULISHO WA TEAM NO SLEEP KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Inaonekana Msanii nyota nchini Uganda Sheebah karungi anaendelea kujitenga na meneja wake wa zamani Jeff Kiwa. Taarifa mpya ni kwamba mrembo huyo amefuta utambulisho wa lebo ya Team No Sleep kwenye bio yake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Lakini pia amemuondoa Jeff Kiwa na mpenzi wake Mutoni Entana kwenye orodha ya watu anaowafuata kwenye mtandao wa instagram. Jeff kiwa na Sheebah hawajathibitisha rasmi kama wamevunja uhusiano wao ila wamekuwa wakitupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii. Ikumbukwe kwa sasa sheebah anaendesha shughuli zake za kibiashara kupitia kampuni yake ya Sheebah business limited huku jeff kiwa akiwa anapromote msanii wake mpya Rahmah Pinky.

Read More