Jennifer Lopez Azua Taharuki AMAs kwa Mabusu ya Jukwaani

Jennifer Lopez Azua Taharuki AMAs kwa Mabusu ya Jukwaani

Mwanamuziki nyota Jennifer Lopez ameibua gumzo kubwa baada ya kufanya onyesho la kuvutia katika Tuzo za American Music Awards 2025, ambapo aliwabusu mcheza densi wa kiume na wa kike jukwaani mbele ya hadhira kubwa mjini Los Angeles. Tukio hilo lilijiri wakati wa onyesho la ufunguzi wa hafla hiyo, ambapo Lopez alionesha ujasiri, ubunifu na utawala wake wa jukwaa kwa zaidi ya dakika tano za mfululizo wa burudani ya moja kwa moja. Kitendo hicho kilizua msisimko mkubwa ukumbini na kusambaa haraka mitandaoni, mashabiki na wachambuzi wa burudani wakitoa maoni mseto. Wengine wamesifu tukio hilo kama ishara ya uhuru wa kisanii na kujiamini jukwaani, huku wachache wakilitafsiri kama jaribio la kuamsha mjadala au kuleta mshangao wa makusudi. Muda mfupi baadaye, Tiffany Haddish, mchekeshaji na mwigizaji maarufu nchini Marekani, ambaye alikuwa mtangazaji wa hafla hiyo, alitoa maoni ya mzaha jukwaani akilichambua tukio hilo kwa ucheshi ulioibua kicheko na shangwe kwa wageni waalikwa. “Our host has just danced to 23 hits in six minutes… and she got all her kisses in. Save a dancer for me, J.Lo. Damn! You ain’t the only one out here single!” Alisema kwa utani mwingi. Tukio hili limethibitisha kuwa Jennifer Lopez bado ni jina kubwa katika burudani ya moja kwa moja, na anaendelea kuvunja mipaka kwa ubunifu wake wa kisanii.

Read More
 Jennifer Lopez Akumbwa na Kesi ya Haki Miliki kwa Kuposti Picha za Paparazzi Bila Ruhusa

Jennifer Lopez Akumbwa na Kesi ya Haki Miliki kwa Kuposti Picha za Paparazzi Bila Ruhusa

Mwanamuziki na muigizaji nyota wa Marekani, Jennifer Lopez, anakabiliwa na madai ya ukiukaji wa haki miliki baada ya kuripotiwa kuposti picha mbili za paparazzi bila kulipia leseni ya matumizi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Billboard, picha hizo zilipigwa wakati Lopez alipokuwa nje ya hafla ya tuzo za Golden Globes mwezi Januari,na baadaye kupostiwa kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii. Hata hivyo, shirika linalomiliki picha hizo linadai kuwa Lopez hakununua haki za kuzitumia, jambo ambalo linakiuka sheria za hakimiliki. Hadi sasa, Jennifer Lopez au wawakilishi wake hawajatoa taarifa rasmi kuhusu tuhuma hizo. Madai hayo yanaongeza msururu wa kesi zinazowakumba mastaa mbalimbali wa Hollywood kwa kutumia picha za paparazzi bila ruhusa, licha ya wao kuwa wahusika wakuu kwenye picha hizo. Kesi hii inaibua tena mjadala mpana kuhusu mipaka ya haki miliki katika enzi ya mitandao ya kijamii, ambapo mastaa wengi huchukulia kuwa picha zao binafsi zinaweza kutumika bila masharti jambo ambalo kisheria haliko wazi.

Read More
 Jennifer Lopez atangaza ujio wa Album mpya

Jennifer Lopez atangaza ujio wa Album mpya

Mwimbaji mkongwe kutoka nchini Marekani, Jennifer Lopez ametangaza ujio wa Album yake mpya ambayo ameipa Jina la “This Is Me… Now” ambayo itatoka mwaka 2023. Album hiyo ina jumla ya nyimbo 13 huku wimbo namba moja ambao ni “This Is Me… Now” ukibeba jina album hiyo. Album hii itazifuata album zake nyingine kama; J.Lo, On the 6, This is Me then, Rebirth, Love Don’t Cost a Thing, A.K.A, Brave na Como Ama una Mujer

Read More
 MUME WA ZAMANI JENIFFER LOPEZ ATOA YA MOYONI KUHUSU NDOA MPYA YA MWANAMAMA HUYO

MUME WA ZAMANI JENIFFER LOPEZ ATOA YA MOYONI KUHUSU NDOA MPYA YA MWANAMAMA HUYO

Aliyewahi kuwa mume wa mwanamuziki Jennifer Lopez, Bw. Ojani Noah halioni penzi na ndoa ya Ex wake JLo na Ben Affleck likidumu, anadai wataachana tu. Ojani Noah amesema ndoa ya wawili hao haitodumu kutokana na tabia ya mwanamama Jennifer Lopez kuwahi kuzama kwenye mapenzi yaani mwepesi wa kupenda kwa haraka. Kupitia mahojiano na Dail Mail, Ex wa JLO, Ojani Noah ambaye alifunga ndoa na Jlo mwaka 1997 na kuachana baada ya miezi 11 baadae, ameliambia gazeti hilo kuwa, “Namtakia yeye na Ben kila la kheri, lakini sishawishiki kama ndoa itadumu, nahisi ni mtu ambaye ataolewa mara 7 au 8. Sioni akitulia na mtu mmoja”. Ikumbukwe, ndoa ya JLO na Ben Affleck ni ndoa ya NNE kwa JLO, walifungua ndoa hiyo Julai mwaka huu.

Read More
 JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA KUTAKA KUACHA MUZIKI

JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA KUTAKA KUACHA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez amefunguka kwamba ilibaki kidogo aachane na muziki kutokana na watu kuzungumzia sana mahusiano yake na kumkosoa sana kuhusu mwili wake. Kwenye Documentary yake mpya “Halftime” ambayo imeanza kuruka kupitia Netflix, Jennifer Lopez amesema muziki wake ulifunikwa na maneno ya watu ambao walikuwa wakimkosoa kwa mengi ikiwemo kukosa makalio makubwa lakini pia kuwa kwenye mahusiano na wanaume tofauti tofauti katika kipindi kifupi. “Nimekulia kwenye mazingira ya Wanawake wenye shape kubwa, hivyo sikuwa na chochote cha kuhofia. Lakini ilikuwa ni ngumu pale unapofikiria watu wanakuona kama kituko. Licha ya yote niliyofanikiwa, hamu yao kuandika stori kuhusu maisha yangu binafsi, kulifunika (Overshadowed) kila kitu kilichotokea kwenye maisha yangu ya muziki. Walikuwa wakisema kwamba Mimi sio mwimbaji mzuri, wala sio mwigizaji mzuri, sio mnenguaji mzuri, sikuwa mzuri kwa chochote na wala sikustahili kuwa hapa.” alikaririwa Jennifer Lopez.

Read More
 JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA JUU YA PETE GHALI ALIYOVISHWA NA BEN AFFLECK

JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA JUU YA PETE GHALI ALIYOVISHWA NA BEN AFFLECK

Mwanamuziki kutoka marekani Jennifer Lopez amefunguka nyuma ya pazia kuhusu tukio la kuvalishwa Pete ya uchumba na Ben Affleck. Katika mahojiano na chombo kimoja cha Habari, Mwanamama huyo amesema haikuwa kama alivyozoea kwani Ben alimkuta mtupu akiwa anaoga kwenye ‘Bubble Bath’ Pete ya Jennifer Lopez inatajwa kuwa na thamani ya ($10 million) ikiwa ni ghali zaidi kuwahi kuvalishwa na wanaume aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano. J-Lo alianza mahusiano na Ben Affleck ambaye ni nyota wa filamu Marekani mwaka 2002 baada ya kutalikiana na mume wake wa pili Cris Judd, waliingia kwenye uchumba November 2002 na kupanga kuoana September 2003 lakini ndoa hiyo iliahirishwa kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari. Uchumba wao ulivunjika rasmi January 2004.

Read More