VDJ Jones akanusha kuwakandamiza wasanii wa Jeshi Jinga
Bosi wa lebo ya muziki ya Superstar Entertainment VDJ Jones amefunguka kuhusu madai ya kuvunja kundi la muziki wa Gengtone Jeshi Jinga. Kwenye mahojiano na Nicholas Kioko amesema madai ya kuinyanyasa kundi hilo kifedha hayana ukweli wowote huku akisema kuwa wasanii wa Jeshi Jinga wenyewe walishindwa kuachia muziki muzuri licha ya kutumia nguvu nyingi kuwatoa kisanaa. VDJ Jones amesema hajutii suala la kusitisha mkataba wa kufanya kazi na wasanii wa kundi hilo kwani walifeli kurudisha shillingi milioni mbili alizowekeza kwenye muziki wao. Sanjari na hilo amemkingia kifua mchekeshaji Eric Omondi kwa kusema kuwa mchekeshaji huyo anaiwazia mazuri tasnia ya muziki nchini Kenya ila wasanii wamefeli kumuunga mkono kwenye harakati za kuleta mabadiliko. Hata hivyo amewataka wasanii wa Kenya waache masuala ya kujihusisha sana na matukio yasiyokuwa na tija kwenye mitandao ya kijamii badala yake waachie nyimbo kali kama namna ambavyo wasanii wa Nigeria na Tanzania wanavyofanya.
Read More