Joel Lwaga Asaini Mkataba na Empire Africa

Joel Lwaga Asaini Mkataba na Empire Africa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania, Joel Lwaga, ametangaza rasmi kusaini mkataba wa usambazaji wa muziki na kampuni kubwa ya kimataifa, Empire Africa. Hatua hii imeonekana kama mwanzo mpya wa ushirikiano wa kibiashara ambao unatarajiwa kupeleka muziki wake katika viwango vya juu zaidi na kumfikisha kwa mashabiki wengi duniani. Kama ishara ya mwanzo wa safari hii mpya, Lwaga ameachia wimbo wake mpya unaoitwa “Saa Hii”, ambao tayari upo kwenye majukwaa yote ya kidigitali duniani. Wimbo huo unakuja na ujumbe wa imani na matumaini, ambao ni utambulisho wa kipekee wa muziki wa Joel Lwaga. Mashabiki wake wamepokea kwa furaha tangazo hilo, wakieleza matumaini makubwa kwamba ushirikiano huu na Empire Africa utaleta mafanikio makubwa zaidi kwa msanii huyo anayejulikana kwa sauti yake yenye kugusa mioyo na nyimbo zenye ujumbe wa kiroho. Kwa kusaini mkataba huu, Joel Lwaga anaungana na orodha ya wasanii kutoka barani Afrika wanaofanya kazi na Empire Africa, kampuni ambayo inajulikana kwa kufanikisha kazi za wasanii katika soko la kimataifa.

Read More
 JOEL LWAGA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

JOEL LWAGA MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injli nchini Tanzania, mtumishi Joel Lwaga ametangaza ujio wa album yake mpya iitwayo “HIGHER AND DEEPER” ambayo inatoka, Julai mosi mwaka huu. Akieleza kuhusu ujio wake huo mpya, Joel Lwaga amesema, album hiyo ina jumla ya nyimbo 15 ambapo baadhi ya hitsong zake zitakuwepo huku zikiwa zimerudiwa kwa kupigwa live. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea “HIGHER AND DEEPER”   ambayo itapatikana Exclusive kupitia mitandao yote ya kustream muziki duniani.

Read More
 JOEL LWAGA ASHINDA TUZO MAREKANI

JOEL LWAGA ASHINDA TUZO MAREKANI

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injli nchini Tanzania, Joel Lwaga ameshinda tuzo za Maranatha zilizotolewa huko Pennsylvania, nchini Marekani. Tuzo hizo ambazo zimefanyika mwishoni mwa wikiendi katika ukumbi wa Grand Gala na kuhudhuruwia na mamia ya watu wakiwemo wadau wa neno la Mungu na waimbaji wenyewe, iliwakutanisha miamba mbalimbali wa tasnia hiyo katika vipengele mbalimbali. Joel lwaga ambaye ameiwakilisha vyema Afrika Mashariki kwenye tuzo hizo katika msimu wake huu wa tatu, ameshinda kwenye kipengele cha (Male Minister Of Excellence). Sanjari na hilo, kwasasa Joel Lwaga yupo mbioni kuachia album yake mpya ambayo itaingia sokoni rasmi tarehe 1 mwezi ujao

Read More