John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto

Mwanamuziki kutoka Marekani ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Grammy John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto mwingine. Kwa mujibu wa Jarida la People, Teigen alijifungua JanuarI 13, mwaka 2023. Legend pia alitangaza taarifa hiyo njema kupitia onesho lake binafsi ambapo aliwaambia wahudhuriaji kwamba “The little baby this morning. What a blessed day.” Familia yao imeongezeka sasa, kwani wana watoto wawili wakubwa, Luna na Miles. Ikumbukwe mwezi Oktoba mwaka 2020 wawili hao waliitia dunia nzima kwenye majonzi baada ya tukio la kumpoteza mtoto wao (Jack) kufuatia Teigen kupata tatizo la kuharibika kwa ujauzito akiwa kwenye kitanda cha kujifungulia.

Read More
 MKE WA JOHN LEGEND AFUNGUKA TUKIO LA HUZINI LILOMTOKEA MIAKA 2 ILIYOPITA

MKE WA JOHN LEGEND AFUNGUKA TUKIO LA HUZINI LILOMTOKEA MIAKA 2 ILIYOPITA

Mke wa msanii John Legend, Chrissy Teigen amefunguka kuhusu tukio la huzuni ambalo lilimtokea miaka miwili iliyopita ambapo alimpoteza mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa. Kwenye mahojiano yake mapya, Teigen mwenye umri wa miaka 36 amesema alimpoteza mtoto huyo kutokana na kutolewa kwa ujauzito (abortion) na sio kuharibika kwa mimba (miscarriage) kama ambavyo ilielezwa. Teigen amesema alishtuka kugundua kwamba alifanyiwa ‘abortion’ ili kunusuru maisha yake kwa mtoto ambaye hakuwa na nafasi tena ya kuishi. Mwanamama huyo amesema ilibidi asizungumze ukweli kutokana na jamii kuona kitendo hicho ni cha ajabu na kisichokubalika, hivyo ikabidi adanganye kwa kusema ujauzito ule uliharibika (miscarriage). Utakumbuka Chrissy Teigen ambaye kwa sasa ni mja mzito amejaliwa kuwapata watoto wawili pamoja na John Legend.

Read More