John Segawa Amshauri Chameleone Kuachana na Bifu na Alien Skin

John Segawa Amshauri Chameleone Kuachana na Bifu na Alien Skin

Mkurugenzi wa filamu nchini Uganda, John Segawa, ameibua mjadala baada ya kutoa maoni yake kuhusu bifu linaloendelea kati ya nyota wa muziki Jose Chameleone na msanii chipukizi mwenye ushawishi mkubwa, Alien Skin. Akizungumza kuhusu mvutano huo, Segawa amesema wazi kuwa Chameleone, kiongozi wa Leone Island, hana nafasi ya kushindana na Alien Skin kwa sababu ya hali yake kiafya na tofauti ya kizazi. Kwa mujibu wa Segawa, Chameleone ni mgonjwa, hafahamu mienendo ya kisasa ya muziki, na kujaribu kuingia katika mapambano na kundi la Fangone Forest kutamletea madhara makubwa. Amefafanua kuwa Chameleone hana nguvu wala nafasi ya kupigana na Alien Skin kwa kuwa vijana ndio wanaoongoza burudani kwa sasa. Aidha, amesisitiza kuwa msanii huyo mkongwe akijaribu kuendeleza bifu hilo, ataishia kupata mateso zaidi badala ya ushindi. Segawa pia ameeleza kuwa bifu hilo linamnufaisha zaidi Alien Skin, kwa sababu msanii huyo bado ni kijana mwenye nguvu na ana miaka mingi ya kufanya muziki mbele yake. Ameongeza kuwa katika hali yoyote ya mvutano, Fangone Forest ingepata ushindi dhidi ya Chameleone kwa sababu ya nafasi yao kubwa katika mwelekeo wa muziki wa sasa.

Read More