Jowy Landa Apinga Kauli ya Spice Diana Kuhusu Mafanikio Bila Kuwa na Hit songs
Mwanamuziki chipukizi kutoka Uganda, Jowy Landa, amejitokeza hadharani kupinga kauli ya Spice Diana kwamba mtu anaweza kufanikiwa katika muziki bila kuwa na nyimbo kali (hit songs). Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni na kituo cha redio, Jowy Landa alisema kuwa mafanikio ya kweli katika muziki hayawezi kupimwa kwa umaarufu wa mtu mtandaoni au mwonekano wa kisanaa pekee, bali kwa uwezo wa kutoa kazi zinazogusa mashabiki na kudumu kwenye chati. “Ni vigumu kusema umefanikiwa kama hauna hata wimbo mmoja ambao watu wanaweza kuuita hit. Mafanikio katika muziki yanatokana na impact unayoacha kwa wasikilizaji. Nyimbo kali huonyesha ubunifu na uwezo halisi wa msanii,” alisema Jowy. Kauli hiyo imeonekana kumlenga moja kwa moja Spice Diana, ambaye hivi majuzi alijinasibu kwamba amefanikiwa katika tasnia ya muziki licha ya kutoachia nyimbo nyingi zilizotamba. Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono Jowy kwa kusema kuwa muziki mzuri ndio unaojenga jina la msanii, huku wengine wakimtetea Spice Diana wakidai kuwa mafanikio ni pana zaidi na si lazima yaambatane na hit songs pekee.
Read More