Wyre, Nameless na Jua Cali kutengeneza bendi ya muziki

Wyre, Nameless na Jua Cali kutengeneza bendi ya muziki

Msanii mkongwe nchini, Wyre amedokeza mpango wa kuunda bendi ya muziki itakayojumuisha wasanii wa kizazi kipya pamoja na wa zamani. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, amepost video akitoa tangazo hilo ambapo amesema wameungana na kutengeneza timu ya malejendari wa muziki. “Kuna nini jamani. Kwa kawaida sifanyi hivi. Imekuwa zaidi ya miaka 20 katika kufanya jambo hili la muziki na nadhani ni kuhusu wakati huu ambao umefika…. Unajua kila kitu kinafikia hatua hiyo ya kufika mwisho. “Kwa hivyo nimeamua.. Tumeamua kuwa tunaunda bendi ya wasanii wa kitambo,” Msanii huyo aliweka wazi hilo huku akihamishia kamera kwa wasanii wengine ambao ni Nameless na Jua Calie pamoja na Kenzo.

Read More
 JUA CALI AWACHANA WASANII WALIOGEUKIA SIASA NCHINI KENYA

JUA CALI AWACHANA WASANII WALIOGEUKIA SIASA NCHINI KENYA

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Jua Cali amewatolea uvivu wasanii ambao wamejiunga na siasa kwa kusema wengi wao hawana vigezo vya kuwa viongozi. Katika mahojiano na SPM Buzz Jua Cali amesema wasanii wamekimbilia siasa kwa sababu wengi wao wana njaa ya kutaka kupata pesa kwa njia ya haraka ila kiuhalisia hawana wito ajenda ya kuwatetea wananchi. Hata hivyo hitmaker huyo wa ngoma ya “Kiasi” amesisitiza kwamba ataendelea kufanya muziki wake hadi mwisho wa dunia huku akisema kuwa hana mpango wa kujiunga na siasa kwani atakuwa anawadanganya wakenya.

Read More