JULIA FOX AWACHANA MATAJIRI, ADAI HAWAPENDI KABISA

JULIA FOX AWACHANA MATAJIRI, ADAI HAWAPENDI KABISA

Kumbe mrembo Julia Fox hakuwa na mapenzi kabisa kwa rapa Kanye West, ni vile tu alipenda pesa zake. Kwenye video ambayo aliiweka TikTok hivi karibuni, mrembo huyo ambaye alikuwa penzini na YE tangu Disemba 2021 hadi Februari 2022 amekiri kuwachukia matajiri ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anatamani hata wasiwepo duniani. “Pesa zinazotoka kwa mabilionea zinatakiwa kurudi kwenye Jamii ambayo iliwafanya wawe matajiri. Huu ndio mtazamo wangu kuhusu mabilionea, hawatakiwi kuwepo kabisa kwenye Jamii yetu. Ndio maana nimekuwa nikiwatumia, sijawahi kupenda yeyote kati yenu ninyi watu.” Alisema

Read More
 UHUSIANO WA KANYE WEST NA MPENZI WAKE JULIA FOX WAINGIWA NA UKUNGU, WAMERIPOTIWA KUACHANA

UHUSIANO WA KANYE WEST NA MPENZI WAKE JULIA FOX WAINGIWA NA UKUNGU, WAMERIPOTIWA KUACHANA

Siku ya Valentine’s Day imeenda vibaya kwa rapa Kanye West na mchumba wake Julia Fox. Wawili hao wameripotiwa kuachana rasmi baada ya miezi miwili ya kuwa penzini. Chanzo cha karibu kimeuambia mtandao wa TMZ kwamba YE na Fox wamebaki tu kuwa marafiki na washirika kwenye masuala mengine. Kuisindikiza siku ya Valentine’s, Kanye West amemtumia Kim Kardashian maua ya kutosha kwenye gari lililofika hadi nyumbani kwake. Rapa kanye west Ni kama bado anatamani kurudiana na Baby mama wake kim kardashian Kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha.

Read More