JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

Rapa kutoka Kenya Juliani amefichua kuwa alipoteza dili mbili kubwa baada ya kuingia kwenye mahusiano ya kimpenzi na Lilian Ng’ang’a mwaka 2021. Akizungumza na Kalondu Musyimi, Juliani amesema makampuni yalioyolenga kufanya nae kazi kipindi hicho yaliingiwa na hofu kutokana na namna watu walivyokuwa wakimshambulia mtandaoni. Juliani hata hivyo ametoa changamoto kwa vyombo vya habari kuwakuza wasanii wa Kenya badala ya kuwapigia simu pale wanapofuatilia habari za udaku. Mapema wiki hii Juliani aliingia kwenye vichwa vya habari za burudani baada ya baadhi ya watumiaji mitandao ya kijamii kumfananisha na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye awali alikuwa akichumbiana na Lilian Ng’ang’a. Walimwengu walienda mbali zaidi na kuhoji ni kwa nini Lilian aliamua kumwacha Mutua mwenye utajiri mkubwa na kuishia kuingia kwenye mahusiano na Juliani ambaye walidai anasuasua kiuchumi.

Read More
 JULIANI AKIRI KUYUMBA KIUCHUMI

JULIANI AKIRI KUYUMBA KIUCHUMI

Mwimbaji Julius Owino almaarufu Juliani amekiri hadharani kuyumba kiuchumi baada ya walimwengu kumkejeli mtandaoni. Katika video aliyochapisha kwenye instastory yake, Juliani amesema kuwa tatizo linalomkabili limechangiwa na hatua ya kutumia fedha zake kufadhili mipango yake bila wafadhili huku akifichua kuwa alichukua mikopo kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya miradi. Aidha amesema changamoto za kifedha anazokumbana nazo kwa sasa zimemfanya akose muda wa kukaa na mtoto wake huku akimshukuru mke wake Lilian Nganga kwa kumuelewa. Katika hatua nyingine mwimbaji huyo amesema kuwa amejipa miaka 10 kutimiza ndoto aliyonayo kwa jamii yake ikiwemo kutengeneza ajira 10,000 na kutoa mikopo kwa wasanii. Juliani, hata hivyo amebainisha kuwa licha ya kuyumba kiuchumi, bado ana uwezo wa kukidhi mahitaji yake ya msingi ambapo amewataka walimwengu kukoma kumfanyia mzaha mtandaoni kuhusiana na hali yake ya kiuchumi kwani inamuathiri kisaikolojia.

Read More
 JULIANI AWAJIBU KISOMI WANAOIPONDA MAHUSIANO YAKE NA LILIAN NGANGA

JULIANI AWAJIBU KISOMI WANAOIPONDA MAHUSIANO YAKE NA LILIAN NGANGA

Hatimaye mwanamuziki Juliani amefunguka kuhusu kinachoendelea mitandaoni kumuhusu mke wake Lilian Ng’ang’a. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameamua kutoa maelezo kuhusu hali yake ya uchumi kwa kuwakejeli wanaomsema vibaya mtandaoni. Rapa huyo ameandika ujumbe anaosema kwamba amefulia kiuchumi ambapo ameenda mbali zaidi na kuwaomba wakenya msaada wa kifedha kupitia paybill ili aweze kumnunulia mtoto wake pampers. “Wase! Nikubaya niko BROKE! mtoi anahitaji pampers. Please send mpesa. Paybill: Business number – 784577 Account- Juliani Chochote unaeza itasaidia. Yours truly, Struggling rapper/entrepreneur”, Ameandika Juliani. Ujumbe huo umezua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa huenda amewajibu kimtindo wanaodai kuwa anaishi maisha ya uchochole huku wengine wakimshushia kila aina matusi kwa hatua ya kukimbia na mke wa Alfred Mutua.

Read More
 LILIAN NG’ANG’A AWACHANA WANAOISEMA VIBAYA NDOA YAKE NA JULIANI

LILIAN NG’ANG’A AWACHANA WANAOISEMA VIBAYA NDOA YAKE NA JULIANI

Mke wa Juliani, Lilian Ng’ang’a ameshindwa kuwavumilia watu wanaozidi kumkejeli mtandaoni kwa hatua ya kuingia kwenye ndoa na mwimbaji huyo. Kilichomuumiza zaidi mrembo huyo ni kitendo cha watu kuhoji kuwa ilikuwa ni fedhea kwake kuacha utajiri wa Alfred Mutua na kisha kukimbilia maisha ya taabu kwa Juliani. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Ng”ang’a ameonekana kukerwa na watu wanaomsema vibaya mtandaoni kwa kuandika ujumbe uliotafsiri kuwa hajutii kumuacha Mutua na kumpenda Juliani ambaye ni mwanamuziki. Lilian ambaye amejaliwa kupata mtoto na Juliani amesema hana muda kabisa wa kupishana na walimwengu ambao hawana shughuli ya kufanya mtandaoni huku akiwataka waendelea kumsema vibaya kwani hana uwezo wa kuthibiti kile wanachomuwazia. Kauli ya Lilian Ng’ang’a inakuja mara baada ya watu kulinganisha utajiri wa mpenzi wake wa sasa Juliani na mume wake wa zamani Alfred Mutua ambaye kwa wakati mmoja aliwahi kuwa gavana wa kaunti ya Machakos.

Read More
 JULIANI AWAPA SOMO WASANII CHIPUKIZI

JULIANI AWAPA SOMO WASANII CHIPUKIZI

Rapa Juliani amewapa somo wasanii chipukizi wanaolaza damu kwenye suala la kuupeleka muziki wao kwenye kiwango kingine. Katika mahojiano yake hivi karibuni Juliani amesema wasanii hao wanapaswa kuchangamkia fursa zilizopo badala ya kulalamika kila mara kuwa wametengwa na jamii inayowazunguka. “Usijidharau msee, because when I look at my career, from where I started to now my fourth album, and the amazing things I’ve done so far, the only constant thing ni nilikuwa najichocha. I had no clue what I was doing but I had the courage to listen to that voice and the courage to boldly take that step.” “Kuna a certain point mtu hufika kwa career when you think you need to do certain things to fit in… but after four-five years of connecting with people I realised kumbe I was contributing to that space just by being myself!” Amesisitiza Hata hivyo amewashauri wasanii wasiongoje wahamasishwe na watu wengine na badala yake wasipambanie ndoto zao wenyewe bila kukataa tamaa hadi pale watakapofanikisha malengo yao. “Sikupatii collabo, una ufala! That’s what everybody [starting out] asks for. Ati ‘Nirushie kacollabo’… No. You have what it takes, I only know about mine, I don’t know about yours,” alimalizia

Read More
 RAPA JULIANI ATAJWA KUSHIRIKI MPANGO WA EISENHOWER FELLOWSHIP

RAPA JULIANI ATAJWA KUSHIRIKI MPANGO WA EISENHOWER FELLOWSHIP

Rapa Juliani amechaguliwa kujiunga na mpango wa Eisenhower Fellowships ambayo inatarajiwa kuanza Aprili 10 hadi mei 18 mwaka wa 2023. Juliani ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kusema kuwa amefarijika kuwa miongoni mwa viongozi wa afrika ambao watasafiri nchini marekani kwa ajili mpango huo ambao umefadhiliwa kwa asilimia kuhudumia mahitaji ya washirika wake. Ushirika wa Eisenhower Fellowships ulibuni mwaka wa 1953 kwa ajili ya kutoa heshima kwa rais Dwight D. Eisenhower kwa mchango wake mkubwa wa kupigania haki za kibinadamu kama kiongozi wa dunia. Utakumbuka Juliani amechagulia kujiunga na ushirika huo kupitia wakfu wake wa Dandora hiphop city na atapata fursa ya kusafiri marekani kwa wiki 4 hadi 6 kupata elimu lakini pia kubadilishana mawazo na watu mbali mbali duniani.

Read More
 JULIANI ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

JULIANI ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

Rapa Juliani ametangaza ujio wa tamasha lake liitwalo Nairobi Startup week ambayo ni mahususi kwa ajili ya wafanyibiashara wadogo na wale wa kadri. Juliani amethibitisha taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram kwa kusema kuwa tamasha hilo la siku tano litaanza rasmi Julai 10 hadi julai 15 huko Waterfront mall jijini Nairobi ambapo itajumuisha maonesho ya bidhaa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali. Rapa huyo amesema nia yake kuja na tamasha hilo ni kwa ajili ya kuonesha na kusherekea umuhimu wa jamii ya wafanyibiashara wadogo na wale wa kadri katika ujenzi wa taifa.

Read More
 RAPA JULIANI APUZILIA MBALI NA MADAI YA KUPEWA KAZI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

RAPA JULIANI APUZILIA MBALI NA MADAI YA KUPEWA KAZI NA MUUNGANO WA KISIASA WA AZIMIO LA UMOJA

Rapa kutoka Kenya Juliani amekanusha kuteuliwa kama afisa mkuu wa masuala ya burudani katika muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja. Kupitia taarifa yake kwenye mitandao yake ya kijamii Juliani amesema madai yanayosambaa mtandaoni kuhusu kuteuliwa kwake hayana ukweli wowote kwa kuwa hajapokea taarifa yeyote kutoka kwa uongozi wa azimio la umoja kuhusu suala la yeye kupewa kazi. Hitmaker huyo wa “Utawala” amesema hajaajiriwa na hana uhusiano wowote na chama chochote cha kisiasa nchini huku akisema ikitokea ameshirikiana na mrengo wowote wa kisiasa ataweka wazi kwa mashabiki wake. Hata hivyo amewataka wakenya kufanya maamuzi ya busara kwa kuwachagua viongozi watakaoleta maendeleo kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu badala ya kudanganywa na wanasiasa wasio kuwa na maono. Kauli ya Juliani imekuja mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kudai sababu za afred mutua kukimbia muungano wa azimio ni kutokana na rapa huyo kupewa wadhfa wa afisa mkuu wa masuala ya buradani ikizingatiwa kuwa mwaka jana rapa huyo aliripotiwa kumpokonya gavana huyo mke wake.

Read More
 RAPPER JULIANI NA LILIAN NG’ANG’A WAFUNGA NDOA YA KIMYA KIMYA

RAPPER JULIANI NA LILIAN NG’ANG’A WAFUNGA NDOA YA KIMYA KIMYA

Rapper Juliani ameripotiwa kufunga ndoa ya kimya kimya na mchumba wake Lilian Ng’ang’a  baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda. Kulingana na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii,Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri imiefanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo wanafamilia pamoja na marafiki. Mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamiii wameonekana kufurahia hatua ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao huku wengine wakiwa na mshangao kwanini ndoa hiyo imekuwa ya siri. Hata hivyo Juliani na Lilian ng’ang’a hawajathibitisha chochote kuhusiana ndoa yao hiyo ila ni jambo la kusubiriwa. Uhusiano wa kimapenzi kati ya rrapa Juliani na Lilian Ng’ang’a ulianza mapema mwaka jana , huku Juliani akithibitisha mahusiano hayo rasmi baada ya ukaribu wake na mrembo huyo gumzo mtandaoni ambapo  wengi walishangazwa na hatua ya msanii huyo kutoka kimapenzi na Lilian Ng’ang’a ikizingatiwa alikuwa mke wa Gavana wa Machakos Alfred Mutua. Ikumbukwe Agosti 15 mwaka 2021 Gavana Mutua na aliyekuwa mke wake Lilian nganga walitumia mitandao yao ya kijamii kuweka wazi kwamba hawapo tena pamoja hii ni baada ya ndoa yao kuvunjika miezi miwili iliyopita.

Read More