Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Juma Jux, ameachia rasmi kazi yake mpya ya muziki, EP iitwayo “A Day To Remember”, kama kumbukizi maalum ya ndoa yake na mkewe mpendwa, Priscy. Kupitia mitandao ya kijamii, Jux ameeleza kuwa mradi huu si kazi ya kawaida, bali ni simulizi ya maisha yao ya upendo, kuanzia mwanzo wa safari yao ya mahaba hadi furaha waliyonayo sasa kama wanandoa. EP hiyo imejaa hisia, utamaduni na usanii wa hali ya juu, ikiwa imeshirikisha mastaa wawili wakubwa: Phyno kutoka Nigeria na D Voice kutoka Tanzania. Jux ameamua kuunganisha ladha ya Afrika Mashariki na Magharibi ili kuwasilisha ujumbe wa upendo unaovuka mipaka ya lugha na mataifa. Kati ya watayarishaji walioweka mikono yao kwenye kazi hii ni S2kizzy, Foxx Made It, na Aykbeats, huku kazi ya mixing na mastering ikifanywa na Lizer Classic, jina kubwa katika ubora wa sauti Afrika. Katika ujumbe wake, Jux hakusita kumshukuru mkewe Priscy kwa kuwa chanzo cha msukumo wa EP hii, pamoja na familia yake, timu nzima ya wasanii na wahusika waliounga mkono kazi hiyo, na mashabiki waliomfuatilia kwa miaka mingi. Amesisitiza kuwa baada ya harusi yao rasmi, atatoa wimbo wa kipekee kama zawadi ya kufunga sura hii mpya ya maisha. EP “A Day To Remember” itapatikana kuanzia usiku wa leo kwenye majukwaa yote ya kidijitali ya kusikiliza muziki. Mashabiki tayari wameonyesha hamasa kubwa, wakisubiri kwa shauku kusikia mchanganyiko wa upendo na sanaa katika kazi hii ya kipekee.

Read More
 Juma Jux kuzindua Album yake mpya Desemba 7 mwaka huu

Juma Jux kuzindua Album yake mpya Desemba 7 mwaka huu

Mwimbaji nyota wa BongoFleva Juma Jux ametangaza kusogeza mbele uzinduzi wa album yake mpya King Of Hearts ambapo sasa uzinduzi huo utafanyika Disemba 7. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jux ameeleza kwamba amefikia maamuzi hayo ili kuhakikisha wasanii wote walioshiriki kwenye album yake wana perform siku ya uzinduzi ndani ya ‘The Super Dome’ Masaki, Jijini Dar es salaam. Lakini pia amebainisha kwamba, siku hiyo ya uzinduzi itajawa na surprise kibao na kuweka historia. “Siku ya tarehe 7 Disemba nataka iwe siku ya Industry nzima kuweka historia. Kuanzia ukumbi ambao itafanyika Show hii, Stage, Mavazi, Performance na kila kitu “, ameeleza Juma Jux.

Read More
 MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA  JUMA JUX ATUA KENYA KWA AJILI YA MEDIA TOUR

MWANAMUZIKI WA BONGOFLEVA JUMA JUX ATUA KENYA KWA AJILI YA MEDIA TOUR

Mwanamuziki Bongofleva, Juma Jux ametua nchini Kenya kwa ajili ya media tour pamoja na kuitangaza brand yake ya African Boy. Akiongea na waandishi wa habari, Jux amesema kuwa dhumuni lake kuu la kutembea Kenya ni biashara lakini pia atawapa mashabiki zake kwa kutumbuiza kwenye moja ya show yake hivi karibuni. “Kuna kazi nimekuja kufanya na pia nimekuja kwa media tour na pia kuna club appearances,” alisema Juma Jux. Utakumbuka kwa sasa Jux anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “I Love You” ambao ameshirikiana na Gyakie kutoka Ghana.

Read More