Justin Bieber Aachia Albamu Mpya “SWAG” Baada ya Miaka Minne

Justin Bieber Aachia Albamu Mpya “SWAG” Baada ya Miaka Minne

Staa wa muziki wa kimataifa, Justin Bieber, ameachia rasmi albamu yake ya saba inayokwenda kwa jina la SWAG, ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu mwaka 2021 alipotoa albamu maarufu ya Justice. Albamu hii mpya imezua msisimko mkubwa miongoni mwa mashabiki, hasa kwa kuwa inamshuhudia Bieber akishirikiana na majina makubwa kama Gunna, Sexyy Red, Cash Cobain, na wengine wengi – wakileta mchanganyiko wa ladha mpya za muziki wa R&B na hip-hop. Kwa mujibu wa wachambuzi wa muziki, SWAG haikuja tu kama albamu mpya, bali kama mwanzo mpya wa safari ya kisanii ya Bieber, akiibuka tena baada ya kipindi kigumu kilichohusisha changamoto za kifedha na mzozo wa kimkataba na meneja wake wa zamani, Scooter Braun. Kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwake, na sasa kupitia SWAG, Justin Bieber anatazamwa kama msanii anayeanza upya kwa mtazamo mpana zaidi wa kimuziki na kibinafsi. Mitandao ya kijamii tayari imefurika mijadala na sifa tele kwa kazi hiyo mpya, huku wengi wakisema albamu hiyo inaonesha ukuaji mkubwa wa kimuziki na kiubinadamu kutoka kwa Bieber.

Read More
 Selena Gomez Amkingia Kifua Hailey Bieber Kisiri Baada ya Shutuma za Justin

Selena Gomez Amkingia Kifua Hailey Bieber Kisiri Baada ya Shutuma za Justin

Mwanamuziki na mwigizaji maarufu, Selena Gomez, ameonekana kuonyesha mshikamano wa kimya lakini wa dhati kwa Hailey Bieber, mke wa zamani wa mpenzi wake, Justin Bieber, kufuatia kauli ya kuumiza aliyotoa Justin kuhusu jarida la Vogue. Hili limetokea baada ya Justin Bieber kufichua kuwa aliwahi kumwambia Hailey kuwa hatawahi pata nafasi ya kuwa kwenye jalada la jarida la Vogue, kauli ambayo wengi waliiona kama ya kubeza ndoto na uwezo wa Hailey katika tasnia ya mitindo Wakati gumzo hilo likiendelea kuchukua nafasi mtandaoni, Selena Gomez alionekana kuonyesha ishara ya kuunga mkono upande wa Hailey kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kwa ku-like chapisho moja kwenye mitandao ya kijamii lililompongeza Hailey kwa ustahimilivu wake. Kitendo hicho kimefasiriwa na mashabiki wengi kama njia ya kuonyesha huruma na mshikamano, licha ya historia yao ya mapenzi na Justin. Mashabiki wameisifu Selena kwa ukomavu na utu alioonyesha, wakisema kwamba hatua yake ni ya kipekee na inathibitisha kuwa wanawake wanaweza kusimama pamoja hata katika hali tata za kihisia. Hadi sasa, Hailey Bieber hajatoa kauli rasmi kuhusu tukio hilo, lakini ishara ya uungwaji mkono kutoka kwa Selena imeonekana kama faraja kwa wengi walioguswa na kauli ya Justin.

Read More
 Justin Bieber Bado Anadaiwa Mamilioni na Meneja Wake wa Zamani Scooter Braun

Justin Bieber Bado Anadaiwa Mamilioni na Meneja Wake wa Zamani Scooter Braun

Nyota wa muziki wa pop Justin Bieber bado anadaiwa mamilioni ya dola na meneja wake wa zamani Scooter Braun, licha ya wawili hao kusitisha rasmi uhusiano wao wa kikazi takribani miaka miwili iliyopita, vyanzo vya karibu na suala hilo vimedokeza. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia vyanzo vya karibu na wasanii hao wawili, deni hilo linahusiana na makubaliano ya kifedha yaliyokuwa ndani ya mkataba wa usimamizi kati ya Bieber na Braun, ikiwa ni pamoja na mgao wa mapato kutoka miradi ya awali ya muziki, matangazo ya biashara, na makubaliano ya udhamini yaliyosainiwa kabla ya kutengana kwao. Scooter Braun aligundua kipaji cha Justin Bieber mwaka 2007 kupitia video ya YouTube na kisha kumsainisha kwenye lebo ya Raymond Braun Media Group (RBMG), ikishirikiana na Island Records. Kwa zaidi ya muongo mmoja, Braun alisimamia safari ya Bieber kutoka kuwa kijana mdogo hadi kuwa miongoni mwa wasanii wanaouza zaidi duniani. Mnamo mwaka 2023, ilithibitishwa kuwa Bieber na Braun hawakuwa tena wakifanya kazi pamoja. Taarifa hiyo iliwashangaza wengi kwenye tasnia ya muziki, hasa ikizingatiwa ukaribu wao wa muda mrefu. Hata hivyo, hakuna upande uliotoa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuvunjika kwa mkataba huo. Chanzo kimoja kilichoomba kutotajwa jina kililiambia shirika moja la habari la burudani kuwa, “Kuna masuala ya kifedha ambayo hayajakamilika tangu walipoachana. Scooter anaamini ana haki ya kulipwa fedha alizopaswa kupata kutokana na kazi aliyofanya kwa miaka mingi.” Ingawa hakuna uthibitisho kuwa suala hilo limefikishwa mahakamani, vyanzo vinasema kuna uwezekano wa kufunguliwa kwa kesi iwapo pande husika hazitafikia makubaliano ya maridhiano. Wachambuzi wa sheria za burudani wanasema kuwa ni jambo la kawaida kwa madeni ya aina hii kuibuka hasa pale ambapo mikataba ilikuwa na vipengele vya malipo ya baadaye (deferred earnings). Mmoja wa wataalamu wa sheria za muziki jijini Los Angeles alisema:  “Mikataba ya usimamizi wa wasanii huwa na vipengele vinavyoruhusu meneja kuendelea kulipwa hata baada ya mkataba kuvunjika, mradi mapato hayo ni matokeo ya kazi iliyofanywa wakati wa usimamizi wao.” Hadi kufikia sasa, Justin Bieber hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu madai haya. Msanii huyo amekuwa akionekana mara chache hadharani na hivi karibuni alionekana kuendelea na maisha ya faragha pamoja na mkewe Hailey Bieber. Katika miezi ya hivi karibuni, Bieber amekuwa akiashiria kurejea kwenye muziki kupitia mitandao ya kijamii, lakini hakutoa tarehe rasmi ya kurejea studio au kutoa albamu mpya.

Read More
 Justin Bieber auza mkusanyiko wa nyimbo zake zote ‘music catalog’

Justin Bieber auza mkusanyiko wa nyimbo zake zote ‘music catalog’

Mwanamuziki Justin Bieber ameuza mkusanyiko wa nyimbo zake zote ‘music catalog’ kwa kiasi cha zaidi ya KSh. Bilioni 24. Bieber ameuza kazi hiyo ya mdomo wake kwa Kampuni ya Hipgnosis Songs Capital ambayo imetangaza rasmi leo kwenye taarifa kwa Waandishi wa habari. Kampuni hiyo inatajwa kununua haki zote za Muziki wa Justin Bieber ikiwemo Publishing copyrights, Master Recordings na neighboring rights. Kwenye Muziki wake, Justin Bieber amefanikiwa kuachia Jumla ya Album (6), EP (2) na kutengeneza zaidi ya nyimbo 70.

Read More
 JUSTIN BIEBER AHIRISHA JUSTICE WORLD TOUR KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA

JUSTIN BIEBER AHIRISHA JUSTICE WORLD TOUR KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA

Justin Bieber ametangaza kuahirisha ziara yake ya “Justice World Tour” kufuatia matatizo ya Kiafya. Ziara hiyo iliyoanza toka Machi mwaka huu na sasa ikiwa imebakiza show 70 hadi mwezi Machi 2023, sasa show hizo zimeahirishwa. Bieber amesema sababu ya kuahirisha maonesho hayo ni kuimarisha afya yake. Baada ya kumaliza onesho lake nchini Brazil, Bieber alisema “Niliposhuka tu Jukwaani, uchovu mzito ulinishika na nikagundua kwamba nahitaji kuiweka afya yangu kama kipaumbele.” alikaririwa JB na kumalizia kwa kusema anabidi achukue mapumziko kwa muda. Mwezi Juni mwaka huu Justin Bieber alimamisha muendelezo wa ziara hiyo kufuatia kukutwa na tatizo la Ramsay Hunt syndrome, ambalo lilipelekea kupoozesha kwa muda upande mmoja wa uso wake. Baada ya mwezi mmoja ziara hiyo ilitangazwa kurejea tena.

Read More
 JUSTIN BIEBER ATANGAZA KUREJEA KWA JUSTICE WORLD TOUR

JUSTIN BIEBER ATANGAZA KUREJEA KWA JUSTICE WORLD TOUR

Staa wa muziki nchini Marekani Justin Bieber anayo furaha kukutangazia kwamba amerejea tena stejini ambapo ziara yake “Justice World Tour” imetajwa kuwa itaendelea tena Julai 31 mwaka huu nchini Italia. Hii inakuwa taarifa njema kwa mashabiki wa Justin Bieber ambao walipigwa na ganzi baada ya tamko la kuahirishwa kwa ziara hiyo mwezi uliopita kufuatia tatizo la Kiafya lililomkumba ambapo alituweka wazi kuwa amepooza kwa muda upande wa kulia wa uso wake.

Read More
 MKE WA MWANAMUZIKI JUSTIN BIEBER AFUNGUKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

MKE WA MWANAMUZIKI JUSTIN BIEBER AFUNGUKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

Mke wa mwimbaji Justine Bieber, Hailey Bieber amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto yaki afya iliyomkabili mwezi uliopita, ambayo ilimfanya moja kwa moja afikiri kuwa amepata ugonjwa wa kiharusi. Utata wa kukumbwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa Hailey, uliishia hospitalini ambako madaktari walibaini kuwa alikuwa na tundu kwenye moyo wake. Kwa mujibu wa ripoti za TMZ inaelezwa kuwa, Hailey alikimbizwa hospitali baada ya kupata dalili zinazofanana na kiharusi na hata baadae madaktari kubaini kuwepo kwa damu iliyoganda kwenye ubongo wake. “TIA”, tatizo linalofahamika kama kiharusi kidogo (a mini-stroke) jambo lililorandana na mawazo yake ya awali punde baada ya kuanza kuumwa. Baada ya uchunguzi wa kina wa madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu, hatimaye Hailey alibainika kuwa na kitu kiitwacho PFO kwa lugha ya kitabibu, yaani tundu/mwanya mdogo kwenye moyo wake. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji ambao ulikwenda vizuri na kumfanya walau kurejea kwenye hali yake kawaida. Hailey anasema amekuwa akitumia dawa za kusaidia damu kutiririka vizuri kwenye mishipa (Blood thinners) kila siku tangu tukio hilo ili kuepuka changamoto hiyo kujirudia tena.

Read More