Justina Syokau avunja ukimya kuhusu gari aliyozawadiwa kwenye Birthday yake

Justina Syokau avunja ukimya kuhusu gari aliyozawadiwa kwenye Birthday yake

Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina syokau amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alizawadiwa gari iliyokuwa imetumika kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Kupitia mitandao yake ya kijamii amesema hatotishwa na maneno ya walimwengu huku akisisitiza kuwa ana furaha mwaka 2023 umeanza vyema kwa zawadi ya nguvu kutoka kwa mpenzi wake. “Aaaa am happy I have a new car Tena present sijanunua nimepewa nashukuru sana . Kama kuna kitu sio mpya sijui, kama kuna kitu mpya mzee sijali what I am happy about is Nimepanuliwa mipaka” “maadui awajafurahi sio vibaya nataka nipeleka maaadui roadtrip mpaka mwezi wa sita,” Aliandika. Kauli ya Justina imekuja mara baada ya wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa gari aina ya Land Cruiser V8 aliyopewa na mchumba wake kama zawaidi kwenye siku yake ya kuzaliwa sio jipya. Justina Syokau aligonga vichwa vya  habari nchini mwaka 2022 alipowadanganya wafuasi wake kuwa alitumia shilling million 2 kufanya upasuaji wa kuongeza makalio yake, madai ambayo yalikuja kubainika kuwa ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni. Kitendo hicho kiliwafanya walimwengu kutoamini, matukio ya mwanamama huyo mtandaoni wakimtaja kuwa mpenda kiki.

Read More
 Justina Syokau awaonya wanawake dhidi ya wanaume wanaowapigia sana simu.

Justina Syokau awaonya wanawake dhidi ya wanaume wanaowapigia sana simu.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Justina Syokau amejitokeza na kuwaonya wanawake dhidi ya kupumbazwa na mapenzi ya mwanzo, akiwataka kujitathmini kwa undani iwapo kweli wanapendwa au ni ngono inayotafutwa kutoka kwao. Katika mahojiano na mtangazaji wa runinga ya NTV Amina Abdi, Justina amedai kuwa ni tamaa ya ngono inayowafanya wanaume wengi kuwapigia wanawake simu mara kwa mara. “Ninadhani wanaume wengine ni tamaa ya ngono inayowafanya wawapigie simu wanawake. Wasichana wanafaa kujiuliza, ukiona anakupigia sana simu, ni ngono anataka ama ni wewe anataka?” Justina alisema kwenye kipindi cha The Trend. Hata hivyo Justina amesema kuwa wapo wanaume walio na nia nzuri wanapowatongoza na kuwachumbia wanawake japo ni adimu kuwapata. “Lakini ninataka kusema kuwa kuna wanaume wazuri hata kama wanavutiwa na hilo, watabaki bado na hata kukuoa,” mwimbaji huyo aliongeza. Justina alikuwa akisimulia ushuhuda wake kwa jinsi alivyojitunza kabla ya ndoa bila kushiriki tendo la ndoa na aliyekuwa mume wake lakini aliachwa tu baada ya hayo yote. “Alikuwa mzuri sana. Alikuwa mzuri. Tulijihifadhi hadi ndoa. Tulikuwa na harusi safi. Sikujua siku moja anaweza niacha,” Justina alisema.

Read More
 Justina Syokau angua kilio kutokana na chuki anayopata kutoka kwa mashabiki

Justina Syokau angua kilio kutokana na chuki anayopata kutoka kwa mashabiki

Mwanamuziki wa Injili Justina Syokau ameumizwa na chuki ambayo amekuwa akiipata hasa baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Twendi Twendi Thilii’. Akizungumza katika mahojiano, Justina Syokau amesema alirekodi wimbo huo chini ya shinikizo ya Roho Mtakatifu lakini Wakenya wameitafsiri vibaya dhana ya wimbo huo. Mwanamuziki huyo ambaye alikuwa akitokwa na machozi akielezea maana ya ujumbe, 2023 ni mwaka wa kupanuliwa, amesema watu ambao hawana ushawishi wa roho mtakatifu watauelewa wimbo huo kwa maana ya kidunia ambayo haikuwa dhamira ya wimbo wake. “Nyimbo zangu ni unabii na ukiziamini mambo yako yatatimia. Magavana wamekuwa wakinipigia simu baada ya wimbo wangu wa 2022. Waliamini maneno hayo na wakachaguliwa.” Justina Syokau amesema amechoka kuimba kutokana na watu kutothamini nyimbo zake na 2023 ni mwaka wa mwisho kutoa wimbo kwani ameamua kufungua kanisa lake na kuwa nabii. “Badala ya Wakenya kuthamini kwamba wana nabii, wamekuwa wakinisema vibaya. Sijui ama nianze kanisa. Mbona hamtaki nisonge mbele, nikiimba Hamnitakii, mnataka niwafanyie nini, mnahangaika mnaomba kila siku ili nipate maudhui ya kuweka hapo, mnaomba mnipe kazi mnaendelea kunitusi.

Read More
 Justina Syokau azua gumzo mtandaoni baada ya kufanya surgery kuongeza makalio

Justina Syokau azua gumzo mtandaoni baada ya kufanya surgery kuongeza makalio

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya Justina Syokau amechukua headlines za mitandao ya kijamii baada ya kushare picha inayomuonesha akiwa na muonekano mpya huku akidai kufanya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio yake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Syokau ameandika  “Hatimaye nimefanikisha lengo langu la kupata makalio makubwa. Napenda muonekano wa mwili wangu mpya,” Haijulikani kama alifanya upasuaji wa kuongeza makalio ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji amehariri picha ili kuonekana ana makalio makubwa. Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita wakati Vera Sidika alipowahadaa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa amefanya upasuaji wa kupunguza makalio kutokana na matatizo ya kiafya, Syokau katika mahojiano na podcast ya mtangazaji Mwende Macharia alisema kuwa hata yeye alikuwa na wazo la kufanya upasuaji ili kuongeza makalio yake. Mwanamama huyo alisema kuwa hatua yay eye kuongeza makalio sio tu kuwavutia wanaume bali ilikuwa njia moja ya kutumia muonekano wa mwili wake kusambaza neon la Mungu.

Read More
 Justina Syokau mbioni kufanya surgery ya shillingi millioni 2 kuongeza makalio.

Justina Syokau mbioni kufanya surgery ya shillingi millioni 2 kuongeza makalio.

Huenda msanii nyimbo za injili Justina Syokau akaenda kufanya ‘Surgery’ kama baadhi ya mastaa wengine walivyofanya ili kuboresha muonekano wake. Hitmaker huyo wa 2020 amesema sio mbaya kwa mtu mwenye uwezo kurekebisha kitu kwenye mwili wake huku akisema kuwa ana lenga kutumia  shillingi millioni 2 za Kenya kuongeza makalio yake. Syokau amesema amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kuwavutia wanaume wengi ambao atawahubiria neno la Mungu ili waweze kubadili mienendo yao na kukumbatia uwokovu. Lakini pia ameweka wazi mpango kupunguza tumbo kwenye mwili wake kwa kuwa vitambi vinasumbua sana wadada, hivyo hata yeye akipata pesa zake ataenda kukitoa.

Read More
 JUSTINA SYOKAU ATAKA SERIKALI YA WILLIAM RUTO KUWASAIDIA WASANII

JUSTINA SYOKAU ATAKA SERIKALI YA WILLIAM RUTO KUWASAIDIA WASANII

Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina Syokau ametoa wito kwa serikali ya Rais William Ruto kutengeneza mazuri kwa wasanii waweze kuingiza kipato kupitia muziki wao. Akizungumza na Nicholas Kioko, Syokau amesema kwa kipindi kirefu wasanii wamekuwa wakisuasua kiuchumi kutokana na ukosefu mifumo rafiki ya kufanya muziki kibiashara zaidi. Hitmaker huyo wa “2020” ametaka serikali kupunguza kodi kwenye baadhi ya huduma ili wasanii wafaidi na sanaa yao kwa kuwa wengi wamekwama kiuchumi licha ya kutumia pesa nyingi kuwekeza kwenye muziki. Sanjari na hilo amekanusha kuiba mashairi ya wimbo wa “Maombi” wake msanii Nadia Mukami na kutumia kwenye wimbo wake mpya ambao aliuimba mahususi kwa ajili ya rais wa tano wa Kenya William Ruto. Mwanamama huyo amesema madai hayo hayana ukweli wowote bali yaliibuliwa na baadhi ya watu wanamuonea wivu kwa mafanikio aliyoyapata kwenye muziki wake.

Read More
 MWIIMBAJI MWENYE UTATA NCHINI JUSTINA SYOKAU AWAONYA WANAUME WANAOMTAKA KIMAPENZI

MWIIMBAJI MWENYE UTATA NCHINI JUSTINA SYOKAU AWAONYA WANAUME WANAOMTAKA KIMAPENZI

Msanii wa nyimbo za Injili mwenye utata nchini Justina Syokau anaendelea kushika headlines za habari za burudani nchini na vituko vyake. Katika mahojiano yake ya hivi karibu na runinga ya Ntv, hitmaker huyo twenty twenty ametoa onyo kali kwa wanaume ambao kwa njia moja au nyingine wamefulia kiuchumi wasijaribu kumtokea kimapenzi. Kwa mujibu wa msanii huyo mwanaume ndiye anafaa kuwa mtoa riziki kwa familia na sio mwanamke huku akiongeza kuwa mwanaume yeyote anayemtegemea mwanamke kulishwa ni mtu mvivu ambaye hatakikani kwa ulimwengu wa sasa. Mwanamama huyo ameenda mbali zaidi na kujitapa kuwa atakuwa anazungumza tu na wanaume wanaoendesha magari makubwa kama Mercedes benz na wanaume wanaomiliki ndege aina ya helicopter. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kukerwa na matamshi ya Justina Syokau ambapo wamemtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye suala la kutoa muziki mzuri badala ya kulazimisha azungumzie kwenye vyombo vya habari wakati nyimbo zake ni mbovu

Read More