Kaa La Moto aachia rasmi Album yake mpya

Kaa La Moto aachia rasmi Album yake mpya

Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ameachia rasmi Album yake mpya, inayokwenda kwa jina la “Mkanda Mweusi.” Album hiyo, ina jumla ya mikwaju 15 huku ndani akiwapa shavu wakali kama AY, Joh Makini, Dully Sykes, Kala Jeremiah, Johnny Skani, Jua Cali, Kelechi Africana na wengine wengi. Hata hivyo  Mkanda Mweusi Album inapatikana Exclusive kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni. Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwake mwaka huu ikizingatiwa kuwa mwezi Mei aliachia Album iitwayo “Leso ya Mekatilili” iliyokuwa na jumla ya nyimbo 12.

Read More
 Kaa La Moto aachia Tracklist ya Album yake mpya

Kaa La Moto aachia Tracklist ya Album yake mpya

Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ameachia Tracklist ya Album yake mpya, inayokwenda kwa jina la Mkanda Mweusi. Album hiyo, ina jumla ya mikwaju 15 huku ndani akiwapa shavu wakali kama AY, Joh Makini, Dully Sykes, Kala Jeremiah, Johnny Skani, Jua Cali, Kelechi Africana na wengine wengi. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Mkanda Mweusi Album,  ambayo itaingia sokoni rasmi Disemba 20 mwaka huu. Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto kwa mwaka huu ikizingatiwa kuwa mwezi mei mwaka huu aliachia Album iitwayo Leso ya Mekatilili iliyokuwa na jumla ya nyimbo 12.

Read More
 MADENI YAMUUMBUA RAPA KAA LA MOTO

MADENI YAMUUMBUA RAPA KAA LA MOTO

Rapa Kaa La Moto ameingia kwenye headlines mara ya kukumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shillingi laki 3 analodaiwa na mwanadada aitwaye Lisa Russell Kwa mujibu wa Lisa Russell Kaa la Moto alimuomba Dola 2,500 atumie kipindi cha corona kwa makubaliano kwamba atamrudishia ila mpaka sasa rapa huyo hajaweza kumlipa deni lake. Aidha amesema licha ya kumpigia simu ili kumuulizia kuhusu deni hilo,rapa huyo pamoja na meneja wake wameingiwa na jeuri kiasi cha kumtishia maisha, hali inayotoa tafsiri kwamba anataka kumdhulumu. Mrembo huyo amesema Kaa la Moto afanikiwa kumlipa shilling elfu 58,700 pekee huku akiahapa kutolegeza msimamo hadi pale rapa huyo atakapokamilisha deni lake la sivyo atazidi kuanika maovu yake. Hata hivyo Kaa la Moto hajajibu tuhuma za kukwepa kulipa deni zilizoibuliwa na Lisa Russell ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 KAA LA MOTO AACHIA RASMI LESO YA MIKATILILI ALBUM

KAA LA MOTO AACHIA RASMI LESO YA MIKATILILI ALBUM

Rapa kutoka Kenya Kaa la Moto ameachia rasmi Album yake mpya inayokwenda kwa jina la Leso ya Mikatilili. Album hiyo ina jumla ya ngoma 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 10 pekee kutoka wakali kama Masauti, Hart the Band, Chikuzee, Mercury, Kigoto, Iddi Singer, Lavido,na Escobaa. Leso ya Mikatilili Album ambayo ina nyimbo kama Nipe Mji, Sisikii Sauti, Karibu mwanangu na nyingine nyingi inapatikana Exclusive kupitia mtandao wa Boomplay Kenya. Hii ni album ya pili kwa mtu mzima Kaa La Moto baada ya kesi ya mwaka wa 2019

Read More
 KAA LA MOTO AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

KAA LA MOTO AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Rapa kutoka Kenya Kaa la Moto ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la Leso ya Mikatilili. Kupitia Instagram yake Rapa huyo amechapisha artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 10 pekee. Kaa La Moto amewashirikisha wakali kama Masauti, Hart the Band, Chikuzee, Mercury, Kigoto, Iddi Singer, Lavido,Escobar, huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Nipe Mji, Sisikii Sauti, Karibu mwanangu na nyingine nyingi. Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Leso ya Mikatilili Album  ambayo itapatikana Exclusive kupitia mtandao wa Boomplay Kenya licha kutoweka wazi tarehe ambayo album hiyo itaingia sokoni. Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto baada ya kesi ya mwaka wa 2019.

Read More
 KAA LA MOTO AWEKA WAZI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

KAA LA MOTO AWEKA WAZI JINA LA ALBUM YAKE MPYA

Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ametaja Jina la Album yake mpya anayotarajia kuachia hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kaa La Moto ameshare cover ya album yake mpya na kutusanua kuwa album yake hiyo ambayo anaiandaa chini studio za Kubwa Studios mjini mombasa Itaitwa LESO YA MEKATILILI. Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album yake ya LESO YA MEKATILILI, Hitmaker huyo wa Dear Hihop hajatuambia tarehe ambayo album hiyo itaingia sokoni rasmi. ila ni jambo la kusubiriwa. Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto baada ya kesi ya mwaka wa 2019

Read More