Kajala Masanja Afichua Alivyohongwa Mamilioni na Wanaume

Kajala Masanja Afichua Alivyohongwa Mamilioni na Wanaume

Muigizaji nyota wa filamu za Bongo, Kajala Masanja, amekiri hadharani kuwa alihongwa mamilioni ya fedha na wanaume waliotaka kutoka naye kimapenzi kipindi ambacho nyota yake ilikuwa imeng’aa kwenye tasnia ya filamu. Akizungumza kupitia podcast ya A List Stars, Kajala amesema licha ya kupata pesa nyingi kutoka kwa wanaume tofauti hakufanya jambo la maana zaidi ya kula bata. Kajala amesema hakuna mwanaume anayeweza kumshtua kwa kumhonga kwa sababu tayari alishapokea kiasi kikubwa cha fedha miaka ya hapo nyuma. Kauli yake iliungwa mkono na mastaa wenzake waliokuwa naye kwenye kipindi hicho, akiwemo Irene Uwoya, Jackline Wolper na Aunt Ezekiel, ambao wamekiri kuwa hali kama hiyo ni ya kawaida kwa mastaa wa kike katika tasnia ya filamu na burudani.

Read More
 Kajala Adai Harmonize Aliwahi Kumsaidi Binti yake Kielimu

Kajala Adai Harmonize Aliwahi Kumsaidi Binti yake Kielimu

Muigizaji wa Bongo Movie Kajala Masanja amefunguka kuwa mwanamuziki Harmonize ambaye kwa sasa ni mume wake aliwahi kumlipia binti yake Paula Kajala ada ya shule alipokuwa akisoma kidato cha pili (Form Two). Kwa mujibu wa Kajala, msaada huo ulikuja katika wakati muhimu wa masomo ya Paulah, jambo analosema linadhihirisha namna Harmonize alivyokuwa tayari kubeba majukumu hata kabla ya mahusiano yao kuwa wazi kwa umma. Mwanamama huyo, amesema uhusiano wao haukuwa wa muda mfupi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani, bali ulianza zamani na ulihusisha pia majukumu ya kifamilia. Hata hivyo, Kajala amesisitiza kuwa aliamua kusema hayo ili kuweka wazi ukweli wa maisha yake binafsi, akibainisha kuwa mengi yalibaki siri kwa muda kabla ya kuwekwa wazi kwa umma.

Read More
 Mchumba wa Harmonize, Kajala Masanja athibitisha kuwa mjamzito

Mchumba wa Harmonize, Kajala Masanja athibitisha kuwa mjamzito

Mchumba wa msanii Harmonize, Kajala Masanja amewafunga midomo walimwengu mara baada ya kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa Bosi wa Konde Gang. Kupitia instastory yake ameposti kipande cha video akilishika tumbo lake linaloonekana ni mjamzito na kuandika; “I can’t wait…” ujumbe ambao umewaaminisha mashabiki kuwa kweli ni mjamzito. Hata hivyo wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii wamepinga taarifa hiyo huku wakihoji kuwa sio tumbo la Kajala ambalo linaonekana kwenye video hiyo bali inaweza ikawa ni Ujauzito wa mtu wao wa Karibu.

Read More