Rapa Kanambo Dede Akamilisha Masomo yake ya Kidato cha Nne

Rapa Kanambo Dede Akamilisha Masomo yake ya Kidato cha Nne

Rapper Kanambo Dede ametimiza hatua muhimu katika maisha yake baada ya kukamilisha rasmi masomo yake ya sekondari. Taarifa za kuhitimu kwake zimethibitishwa na msanii na mkurugenzi wa Kaka Empire, King Kaka, ambaye ameposti kipande cha video akiwa na Kanambo na kusisitiza kuwa mashabiki wajiandae kupokea muziki mzuri kutoka kwake. King Kaka ameonyesha matumaini makubwa kwa nyota huyo chipukizi, akisema uamuzi wake wa kurudi shule na kutanguliza elimu ni jambo la kupongezwa. Kanambo alirejea shuleni kupitia msaada na usimamizi wa Kaka Empire baada ya kupambana na umasikini na changamoto za ujauzito wa mapema.

Read More
 KANAMBO DEDE ARUDI SHULENI KUKAMILISHA MASOMO YAKE YA SEKONDARI

KANAMBO DEDE ARUDI SHULENI KUKAMILISHA MASOMO YAKE YA SEKONDARI

Female rapper kutoka Kenya Kanambo Dede amerudi tena shuleni kuendeleza masomo yake ya upili baada ya kuacha shule miaka kadhaa iliyopita. Rapa huyo ambaye alipata umaarufu nchini baada ya video yake kusambaa akiwa anachana mistari ya muziki wa hiphop aliacha shule kutokana na umaskini nyumbani kwao lakini pia mimba aliyoipata akiwa mchanga. Akizungumza na mungai eve wakati wa uzinduzi wa tamthilia yake iitwayo Kamtupe nimsanye kanambo amesema ilikuwa ni matamanio yake kumaliza shule na kufanikisha ndoto zake maishani ” Since I moved out of Kayole, I felt I needed to go back to school and lay a foundation for my dreams since I feel I messed up in the past.” Rapa huyo mchanga amewahimiza wanafunzi  ambao tayari wapo mashuleni kutia bidii kwenye masomo huku akisema maisha mtaani ni magumu hivyo kwa wale ambao wana uwezo wa kupata elimu wachangamkie hiyo fursa. Hata hivyo amesema atafanya kila awezalo kuhakikiaha anasoma lakini pia kwa upande mwingine anaendeleza kazi zake za muziki. Ndoto za Kanambo dede kurudi shule imefanikishwa na uongozi wake wa Kaka Empire ambao umekuwa ukimuunga mkono kwenye shughuli zake za kimuziki ambapo mpaka ameshaachia ngoma tatu ambazo ni One Day, Wallahi, na Nataka Tena.

Read More