JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

Orodha ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza pesa nyingi zaidi mwaka wa 2021 imetoka na jina la Jay-Z lipo namba 1. Jay Z ametajwa kuingiza kiasi cha shilling billion 51.2 za Kenya  ambazo zimetokana na pato la baada ya kuuza hisa zake nyingi za mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square Ink, kwa takriban shilling billion kiasi cha shilling billion 34.4 za Kenya. Lakini pia Jay Z alikunja mkwanja mrefu mwaka jana baada ya kampuni ya LVMH kununua nusu ya hisa za Kinywaji chake, cha Armand de Brinac. Kwa upande wa Kanye west ambaye amekamata nafasi ya pili kwa shilling billion 28.5 za Kenya, pato lake kubwa limeendelea kuingia kupitia bidhaa za Yeezy. Wasanii wengine waliongiza pesa nyingi mwaka wa 2022 ni pamoja na Diddy ambaye alikamata nafasi ya tatu kwa shilling billion 8.5 akifuatwa na drake aliyeingiza kiasi cha shilling billion 5.7 huku tano bora ikifungwa na mtu mzima wiz khalifa ambaye aliingiza kiasi cha shilllingi billion 5.1 za Kenya. HIP-HOP’S TOP EARNERS 2021 JAY-Z – $470 million Kanye West – $250 million Diddy – $75 million Drake – $50 million Wiz Khalifa – $45 million Travis Scott – $38 million DJ Khaled – $35 million Eminem – $28 million J. Cole – $27 million Birdman – $25 million Doja Cat – $25 million Tech N9ne – $25 million

Read More
 KANYE WEST KURITHI NAFASI YA VIRGIL ABLOH KAMA MKURUNGEZI WA LOUIS VUITON

KANYE WEST KURITHI NAFASI YA VIRGIL ABLOH KAMA MKURUNGEZI WA LOUIS VUITON

Rapa kutoka Marekani Kanye West anatajwa kama mrithi wa nafasi ya marehemu Virgil Abloh kama Mkurugenzi wa ubunifu kwenye kampuni ya Louis Vuitton. Jarida la The Sun limeripoti kwamba Kifo cha Abloh kilimgusa sana YE kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa zaidi ya miaka 12, hivyo kukaa kwenye kiti chake pale Louis Vuitton anajihisi kama atakuwa amelipa deni la urafiki wao kwa kukamilisha ambacho alikuwa amekiacha. Virgil Abloh alifariki dunia Novemba 28 mwaka huu kwa ugonjwa wa Saratani ambao alikuwa akipambana nao kwa miaka miwili. Abloh alikutana na YE mwaka 2009 wakati wakifanya kazi kwenye kampuni ya Fendi mjini Roma nchini Italia. Mwaka 2018 marehemu Abloh alitangazwa kuwa Mkurugenzi wa ubunifu upande wa mavazi ya Kiume kwenye kampuni ya Louis Vuitton.

Read More