KANYE WEST ATAKA KUMALIZA BIFU YAKE NA DRAKE

KANYE WEST ATAKA KUMALIZA BIFU YAKE NA DRAKE

Staa wa muziki Hiphop kutoka Marekani  Kanye West amejitokeza hadharani kuomba kumaliza tofauti zake na Drake. Kanye West amefikia maamuzi hayo akiwa na lengo la kumshawishi Drake aungane naye wafanye tamasha la pamoja Disemba 7 mwaka huu kwa lengo la kumsaidia Larry Hoover aachiwe huru kutoka gerezani ambapo anatumikia kifungo cha maisha tangu mwaka 1973. “Nimetengeneza video hii kuzungumzia yote yanayo endelea kati yangu na Drake. Wote sisi tumekuwa tukitupiana maneno na sasa ni muda wa kumaliza tofauti zetu. Ninamuomba Drake aungane na Mimi Jukwaani mnamo Disemba 7 Jijini Los Angeles kama mgeni maalum kwa ajili ya kuziunganisha album mbili bora za mwaka kwa lengo kuu la kupaza sauti za kumuacha huru Larry Hoover.” amesema Kanye West. Larry Hoover ambaye ni muanzilishi wa genge maarufu la kihuni na kihalifu nchini marekani liitwalo Gangster Disciples alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo mauaji, kupanga njama za uvamizi na uporaji pamoja na makosa mengine ya jinai. Ikumbukwe kuwa wawili hao wapo kwenye bifu zito kwa sababu kuna kipindi Drake aliwahi kusema kuwa yupo kwenye mahusiano na ex wa rapa Kanye West ambaye ni Kim Kardashian na kwa kuthibitisha hilo alim-follow Instagram pamoja na kutoa ngoma yake ya “In My Feeling” akimuimba “kiki” ambalo ni jina lingine la mrembo huyo. Lakini pia hivi karibuni Kanye West ali-share location ya mjengo wa Drizzy huko Toronto Canada na kisha kuifuta post hiyo huku Drake akimdhihaki kwa kujibu kupitia video aliyoi-share kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akicheka.

Read More