KAPA CAT AKOSOA SERIKALI KUWAFUNGIA WASANII KUFANYA SHOWS MASHULENI

KAPA CAT AKOSOA SERIKALI KUWAFUNGIA WASANII KUFANYA SHOWS MASHULENI

Mwanamuziki kutoka Uganda Kapa Cat ameitaka wizara ya elimu kutoingilia namna wasanii wanavyovalia mavazi yao. Akizungumza kwenye moja ya show yake Kapa Cat amesema hatua ya wizara hiyo kuwafungia wasanii kufanya show zao mashuleni, inawanyima uhuru wa kuwa wabunifu kwenye suala la kuendeleza sanaa yao. Utakumbuka mwezi mmoja uliopita wizara ya elimu nchini iliwapiga marufuku kutotumbuiza mashuleni kutokana na baadhi ya wasanii wa kike kuvalia mavazi yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii. Hata hivyo mpaka sasa wasanii hawajui ni lini hasa serikali itawaruhusu kutumbuiza mashuleni.

Read More
 KAPA CAT AKIRI HADHARANI KUCHUKIA MIPIRA YA KONDOMU

KAPA CAT AKIRI HADHARANI KUCHUKIA MIPIRA YA KONDOMU

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo Kapa Cat amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kukiri hadharani kuwa anachukia kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa. Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni mrembo huyo ambaye anadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda amesema anafadhalisha kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga kwa kuwa mipira ya kondomu humwasha sana kwenye sehemu zake za siri. Hitmaker huyo wa ngoma ya “You Guy” ameenda mbali na kudai kuwa kipindi cha nyuma alikuwa na mazoea ya kupima HIV kila baada ya miezi mitatu lakini daktari alipogundua yuko njia panda kiafya alimshauri kujenga tabia ya kujua hali yake kila baada ya miezi miwili. Kapa Cat alipata umaarufu kwenye muziki wake mwaka wa 2018 kupitia wimbo wake uitwao “Sikyo” na tangu wakati huo amekuwa akisuasua kwenye suala la kuachia hitsongs.

Read More
 KAPA CAT AMBURUZA PROMOTA MAHAKAMANI KWA KUCHOCHEA MASHABIKI KUAHARIBU GARI LAKE

KAPA CAT AMBURUZA PROMOTA MAHAKAMANI KWA KUCHOCHEA MASHABIKI KUAHARIBU GARI LAKE

Mwanamuziki kutoka Uganda Kapa Cat, ametishia kumfungulia mashtaka promota mmoja huko Bugiri kwa madai ya kuwachochea mashabiki kuaharibu gari lake. Kapa Cat amesema promota huyo anayefahamika kwa jina la Kim aliwaambie mashabiki kuwa hajafaki eneo la show jambo ambalo liliwafanya mashabiki kuzua vurugu na kuanza kuaharibu gari lake alilokuwa ameegesha karibu ukumbi wa burudani. Hata hivyo amelaani tukio hilo kwa kusema kwamba show ya promota huyo ilikuwa mbovu kuwahi kuaandaliwa nchini uganda ambapo amedai anaelekea mahakamani kufungulia kesi  kwa kumsababishia hasara ikizingatiwa kuwa alikuwa amefika eneo la show mapema kwa ajili ya performance yake.

Read More