KAROLE KASITA AKANUSHA KUWA NA UJA UZITO WA FFEFE BUSI
Siku kadhaa zilizopita video iliokuwa ikionesha uja uzito wa msanii Karole Kasita ilivuja na kusambaa mtandaoni. Walimwengu kwenye mitandao ya kijamii walianza kuhusisha uja uzito huo na rapa Ffefe Busi ambaye walimtaja kama mhusika mkuu kutokana na ukaribu wake na mrembo huyo. Sasa Karole Kasita ameibuka na kukanusha madai yao kwenye mahojiano yake mapya kwa kusema kwamba hajawahi kuwa na mahusiano yeyote ya kimapenzi na Ffefe Busi kwani ni mshikaji wake wa karibu. Hitmaker huyo wa “You” amesema anayehusika na uja uzito wake ni mtu anayemheshimu, hivyo hatoweka wazi maelezo ya uja uzito wake kwa umma kwani hapendi kuanika mambo yake ya faragha hadharani.
Read More