RAPA WA KENYA KAYCCY ATEULIWA KUSHIRIKI 2022 XXL FRESHMAN 10 SPOT MAREKANI
Rapa wa Kenya anaishi nchini Marekani KayCyy ameteuliwa kuwania nafasi ya kuingia katika orodha ya wasanii 10 watakaoshirikishwa kwenye 2022 XXL Freshman 10th Spot, listi ya marapa 10 bora ambayo hutolewa kila mwaka na jarida la New York Hiphop Magazine siku chache baada ya kutambuliwa na waandaji wa tuzo za Grammy. Rapa huyo ambaye anafahamika kama Mark Makora Mbogo atachuana na marapa wengine 98 kutoka Marekani kupata nafasi ya kushirikishwa kwenye kava ya gazeti la muziki wa hiphop la New york Hiphop Magazine. Orodha ya 2022 XXL Freshman 10th Spot ina historia ya kuwaangazia marapa kumi bora ambao wanafanya vizuri kila mwaka hasa wanaochipukia kwenye kiwanda cha muziki wa hiphop nchini marekani. KayCyy anakuwa msanii kwanza kutoka Afrika mashariki kuteuliwa kushiriki kwenye orodha ya 2022 XXL Freshman 10th Spot, na tayari mashabiki wameanza mchakato wa kupiga kura kwa wasanii wao wanaowapenda.
Read More