KAZ AWAJIBU WANAOMTISHIA MTANDAONI

KAZ AWAJIBU WANAOMTISHIA MTANDAONI

Mwanamuziki Kaz Lucas amewajibu wanaotaka kuanika picha zake za utupu baada ya kukiingia kifua klabu moja ya usiku iitwayo Alchemist iliyoko jiji Nairobi kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram amesema ameshangazwa na namna watu wameanza kumdhalalisha kutokana na maoni yake juu night club hiyo huku akisema yeyote anayetaka kuchapisha picha zake za utupu ana ruhusa ya kufanya hivyo kwa kuwa hajutii matamashi aliyotoa kuhusu Alchemist. Kauli ya Kaz imekuja mara baada ya watu kumshambulia alipoanza kuwalaumu watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kuchochea serikali kufungwa Alchemist ambayo ilikuwa imetoa ajira kwa wakenya wengi. Wiki iliyopita video ilisambaa mtandaoni ikimuonyesha jamaa moja mwenye asili ya kiafrika akitimulia kwenye eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya wazungu jambo ambalo lilipelekea wakenya kukashifu vikali kitendo hicho cha kibaguzi.

Read More
 KAZ LUCAS AWAPA SOMO WATUMIAJI WA MITANDAO KWA KUCHANGIA KUFUNGWA KWA ALCHEMIST

KAZ LUCAS AWAPA SOMO WATUMIAJI WA MITANDAO KWA KUCHANGIA KUFUNGWA KWA ALCHEMIST

Mwanamuziki Kaz Lucas amesikitishwa na hatua ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kupelekea eneo la burudani la Alchemist liloko jijini Nairobi kufungwa kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Kaz amedai kufungwa kwa eneo hilo kumepelekea maelfu ya wakenya kukosa kazi jambo ambalo amesema limetokana na baadhi ya watu kwenye mitandao ambao hawana huruma kwa shughuli za watu. Aidha amewataka wakenya kutumia mitandao ya kijamii kwa busara badala ya kuwaharibia watu riziki yao kutokana na wao kuamini uvumi unaoenezwa na wambea. Kauli ya Kaz Lucas imekuja mara baada ya Alchemist kufungwa kwa madai ya kuwabagua wateja wao kwa misingi ya rangi. Mapema wiki hii video ilisambaa mtandaoni ikimuonyesha jamaa moja mwenye asili ya kiafrika akitimulia kwenye eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya wazungu jambo ambalo lilipelekea wakenya kukashifu vikali kitendo hicho cha kibaguzi.

Read More