Kelechi Africana akanusha kumtelekeza mtoto wake

Kelechi Africana akanusha kumtelekeza mtoto wake

Msanii Kelechi Africana amepuzilia mbali tuhuma za kumtelekeza mtoto wake. Kelechi amesema madai ya kumkimbia mtoto wake hayana msingi wowote ikizingatiwa kuwa amekuwa akitekeleza majukumu yake kama baba. Hitmaker huyo wa “Nimechoka” amesema baby mama wake anatafuta umaarufu kupitia jina lake kwa kutengeneza lawama ambazo hazina ukweli. Kauli ya Kelechi inakuja mara baada ya taarifa kusambaa mtandaoni kuwa amefikishwa kwenye mahakama ya watoto ya Tononoka kwa kosa la kumtelekeza mtoto wake. Awali baby mama wake aitwaye Shinaz Shaz alidai kwamba Kelechi amekuwa akikwepa majukumu yake kama baba, jambo lilomfanya amtumie maafisa wa polisi alipokuwa kwenye show huko Voi mwisho mwa juma lilopita.

Read More
 Kelechi Africana akamatwa na polisi

Kelechi Africana akamatwa na polisi

Msanii kutoka nchini Kenya Kelechi Africana anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumtelekeza mtoto wake. Akizungumza na Msenangu FM baby mama wa msanii huyo anayejulikana kama Shinaz Shaz amedai kwamba msanii huyo amekwepa majukumu yake kama baba. Shaz anasema jambo hilo lilimfanya amtumie maafisa wa usalama alipokuwa kwenye show huko Voi siku ya ijumaa wiki iliyopita. Msanii huyo tayari amefikishwa kwenye mahakama ya watoto ya Tononoka.

Read More
 KELECHI AFRICANA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

KELECHI AFRICANA AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa muziki nchini Kelechi Africana ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la The Sound Chief Experience. The Sound Chief Experience ina jumla ya nyimbo 16 za moto ambazo amezifanya bila kumshirikisha msanii yeyote. Album hiyo ambayo inapatikana kwenye app ya Hustle Sasa ina nyimbo kama Sorry, Kabisa, Friend, Njoo, Mine na nyingine nyingi. Hii ni album ya kwanza kwa mtu mzima Kelechi Africana ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020 aliwabariki mashabiki zake na ep iitwayo Keep It Fleek ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju 4 ya moto.

Read More