Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Mwanamuziki Kelly Rowland amemkingia kifua Chris Brown mbele ya mashabiki ambao walianza kumzomea kwenye utoaji wa Tuzo za (American Music Awards) usiku wa kuamkia leo. Baada ya kumtangaza kama mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa R&B, Breezy hakuwepo ukumbini na Kelly alilazimika kumchukulia Tuzo hiyo, lakini wakati akizungumza, mashabiki walianza kumzomea. Kelly Rowland aliwakatisha na kuyasema mazuri ya Chris Brown. Utakumbuka siku chache kuelekea utolewaji wa Tuzo za American Music Awards, Waandaaji wa tuzo hizo waliifuta performance ya Chris Brown ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kutoa heshima kwa Michael Jackson.

Read More
 KELLY ROWLAND AFUNGUKA KUHUSU KUNDI LA DESTINY’S CHILD KURUDI KWENYE MUZIKI

KELLY ROWLAND AFUNGUKA KUHUSU KUNDI LA DESTINY’S CHILD KURUDI KWENYE MUZIKI

Aliyekuwa member wa kundi la Destiny’s Child, Kelly Rowland  amenyoosha maelezo kufuatia uvumi kwamba kundi la Destiny’s Child lipo mbioni kuerejea kwa ajili ya kufanya muziki mpya na tamasha lao la muziki. Kupitia mahojiano na Entertainment Tonight, Kelly Rowland amesema kundi hilo kwa sasa linaendelea kuweka mikakati ya kurejea kwenye muziki huku akiwataka mashabiki wao kukaa mkao wa kula kuwapokea. “Tunampenda kila mtu sana ila nadhani jambo hili linastahili kuwa la kushtukiza zaidi, kila kitu kitapangwa ila mtashtukizwa tu, itakuwa surprise mzuri”. Kundi hilo linaloundwa na mastaa watatu akiwemo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams lilivunjika  mwaka 2006 na kila msanii akaendelea kufanya kazi zake za muziki kama msanii wa kujitegemea.

Read More