AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

Nyota wa muziki nchini Akothee amerejea tena katika hoteli ya kifahara ya Kempinski,ikiwa ni wiki mbili imepita baada ya kuhapa kutokanyaga kwenye hoteli hiyo. Hatua hiyo ya Akothee imeonekana kuwakera wakenya kwenye mitandao ya kijamii wengi wakisema msanii huyo ni mnafiki na kauli  chafu aliyoitoa juu ya hoteli ya Kempinski haiwezi haribu brand ya hoteli hiyo. Akothee alikuwa anahudhuria hafla ya kusherekea mafanikio ambayo kinara wa ODM Raila Odinga ameiletea taifa la Kenya wikiendi hii iliyopita. Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita Akothee aliichana hoteli ya kifahari ya Kempinski iliyoko jijini Nairobi kwa madai ya kuwa na uongozi mbaya kwani mameneja wa hoteli hiyo walimsumbua sana kipindi anasherekea mwaka mmoja wa kuzinduliwa kwa wakfu wake wa Akothee Foundation katika hoteli hiyo.

Read More