Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii Marya Alazwa Hospitalini Baada ya Kiharusi, Aomba Msaada wa Kifedha

Msanii maarufu wa Kenya, Marya, anayekumbukwa kwa kibao chake maarufu Chokoza alichomshirikisha Avril, kwa sasa amelazwa hospitalini baada ya kupata kiharusi (stroke). Taarifa zilizotolewa na marafiki wake wa karibu, akiwemo msanii Avril, zinaeleza kuwa Marya amekuwa akiendelea kupokea matibabu hospitalini kwa muda, na anatarajiwa kuruhusiwa hivi karibuni. Hata hivyo, hali yake bado si nzuri kwani amepooza upande mmoja wa mwili wake, hivyo atahitaji huduma ya karibu ya nyumbani. Katika ujumbe wake, Avril alieleza kuwa Marya anahitaji msaada wa kifedha ili kuandaa mazingira salama na yenye huduma bora nyumbani. Msaada huo unahitajika kwa ununuzi wa vifaa maalum kama kitanda cha hospitali, kiti cha magurudumu, godoro maalum, na vifaa vingine vya matibabu. Avril pia alitoa wito kwa mashabiki na Wakenya kwa ujumla kuendelea kumuombea Marya ili apate nafuu na aweze kurejea katika hali yake ya kawaida. Marya aliwahi kuwa mmoja wa wasanii wakubwa nchini, akijizolea umaarufu kupitia Chokoza na nyimbo nyingine zilizowahi kutamba. Ingawa amekuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki, mchango wake bado unakumbukwa na wengi. Kwa sasa, jamii ya wanamuziki, mashabiki na Wakenya kwa jumla wanahimizwa kuungana kwa moyo wa utu na mshikamano, ili kumpa Marya matumaini na msaada anaohitaji katika kipindi hiki kigumu. Kwa yeyote anayetaka kuchangia, mchango unaweza kutumwa kupitia nambari ya simu 0723 207 376 kwa jina la Lilian Miring’u.

Read More