Wachambuzi Wabashiri GNX ya Kendrick Kushinda Album Bora ya Mwaka

Wachambuzi Wabashiri GNX ya Kendrick Kushinda Album Bora ya Mwaka

Wachambuzi wa muziki duniani wanaitabiria album mpya ya Kendrick Lamar, GNX, kushinda tuzo ya Album Bora ya Mwaka kwenye Grammy 2026. Ikiwa atashinda, Kendrick atavunja rekodi ya kuwa msanii wa rap (Solo) wa kwanza kushinda kipengele hicho. Ushindi wa GNX utaimarisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wa hip-hop wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, huku akikaribia kuvunja rekodi ya Jay Z na Kanye West kwa kushinda Grammy nyingi zaidi kwa rapper. Baadhi ya hit songs kutoka kwenye album hiyo zimechochea imani kuwa GNX ni bora. Kwa ujumla, GNX ni album iliyojaa uandishi wa hali ya juu, inafanya vizuri kwenye mauzo ndiyo maana wengi wanaamini, Grammy 2026 itashinda kipengele cha Album bora.

Read More
 Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Mtayarishi mkongwe wa muziki nchini Marekani Dr. Dre, amefunguka sababu za kuchagua upande kwenye bifu ya Drake na Kendrick Lamar iliyotikisa ulimwengu wa muziki wa Hiphop duniani. Akizungumza kwenye podcast ya The Unusual Suspects With Kenya Barris and Malcolm Gladwell, Dr. Dre ameeleza kuwa hakuvutiwa na hatua ya Drake kumshambulia Kendrick Lamar pamoja na familia yake. “Ninapenda wimbo wa  ‘Not Like Us’. Lakini niliposikia Drake akisema mambo mabaya kuhusu mke wa Kendrick na watoto wake, nikasema ‘Ah, adios!’”, Alisema Dre. Kauli ya Dr. Dre inakuja muda mfupi baada ya Drake kufungua kesi dhidi ya Universal Music Group kuhusu wimbo ‘Not Like Us’, ambao una mashambulizi makali dhidi yake. Hii si mara ya kwanza Dre kuzungumzia ‘Not Like Us’. Novemba mwaka jana, aliusifu wimbo huo kwa kusema kuwa umeleta mshikamano mkubwa kwa muziki wa Hiphop nchini Marekani.

Read More
 Kendrick Lamar atumia sura za J Cole, Future na King James kwenye show yake

Kendrick Lamar atumia sura za J Cole, Future na King James kwenye show yake

Rapa Kendrick Lamar ameendeleza ubunifu wake wa kutumia sura za watu mbalimbali kwenye mwili mmoja ‘Deepfake’ katika kufikisha ujumbe anaoutaka. Kama alivyofanya katika wimbo wake wa “The heart part 5” uliopo kwenye album yake ya “Mr Morale & the Big Steppers” ambapo alitumia sura za watu mbalimbali maarufu kama Kanye West, Will Smith na Nipsey Hussle. Rapa huyo ametumia ubunifu huo katika kutambulisha ngoma yake ya “Saviour” kwenye tamasha lililofanyika Paris wiki hii ambapo ametumia sura ya J Cole, Future pamoja na Lebron James.

Read More
 Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa  Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Rapa Kendrick Lamar ameibuka mshindi wa kipengele cha Hip-Hop Artist Of The Year kwenye Tuzo za BET Hip-Hop 2022 ambazo zinatolewa usiku wa kuamki leo nchini Marekani. Kendrick Lamar pia ameondoka na ushindi kwenye vipengele vya Lyricist Of The Year, Best Hip Hop Video “Family Ties”, Best Live Performer na Hip Hop Album Of The Year (Mr. Morale & The Big Steppers) Kwa upande mwingine Rapa 50 Cent ameibuka mshindi wa Tuzo ya ‘Hustler Of The Year’ akiwaangusha DJ Khaled, Drake, Cardi B, Jay-Z, Kanye West na Megan Thee Stallion. Kolabo ya Future, Tems na Drake “Wait For You” imeshinda Tuzo ya Best Collaboration kwenye Tuzo za BET Hip Hop 2022.

Read More
 BOSI WA TOP DAWG AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA KENDRICK LAMAR

BOSI WA TOP DAWG AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA KENDRICK LAMAR

Rais wa Top Dawg Entertainment, Terrence “Punch” Henderson amesema bado anajali kuhusu maendeleo ya rapa Kendrick Lamar licha ya kuachana na Label hiyo mwaka huu. Akizungumza na podcast ya My Expert Opinion Punch amesema “Ninajali kuhusu yeye kiujumla kama binadamu. Ni kama kutumia mfano wa mtoto, kuna wakati wataenda nje, huwezi kwenda nao kila wanapoenda. Wataenda nje na kutafuta uzoefu.” huku akikazia kwamba, hata akikwama basi asisite kumpigia simu kwa ushauri. Utakumbuka Kendrick Lamar aliondoka kwenye Label ya Top Dawg Entertainment ambayo aliitumikia kwa takriban miaka 17 punde tu baada ya kuachia album yake Mr. Morale and the Big Steppers.

Read More
 KENDRICK LAMAR YUPO NCHINI GHANA KWA KUELEKEA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA USIKU WA LEO

KENDRICK LAMAR YUPO NCHINI GHANA KWA KUELEKEA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA USIKU WA LEO

Tovuti mbali mbali nchini Ghana zimeripoti kwamba Kendrick Lamar yupo nchini humo kuelekea uzinduzi wa Album yake mpya “Mr. Morale & The Big Steppers” usiku wa Mei 13. Kendrick ameonekana akiwa na timu yake wakipata chakula kwenye mgahawa mmoja Jijini Accra. Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya vyanzo vya habari, Kendrick Lamar yupo nchini Ghana kwa ajili ya Listening Party ya Album yake ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na kampuni moja kubwa ya muziki. Lengo lingine la ujio wake nchini humo ni ku-shoot Documentary kwa ajili ya Album yake.

Read More
 KENDRICK LAMAR KUACHIA ALBUM YAKE MPYA IJUMAA HII

KENDRICK LAMAR KUACHIA ALBUM YAKE MPYA IJUMAA HII

Baada ya ukimya wa takribani miaka 5, rappa Kendrick Lamar anarudi kwenye masikio yako. Kupitia mitandao yak ya kijamii Lamar ametangaza rasmi ujio wa Album yake mpya iitwayo “Mr. Morale & The Big Steppers” ambayo itaachiwa rasmi Kesho Mei 13. Rapa huyo kutoka marekani ameachia Cover ya Album yake mpya “Mr. Morale & The Big Steppers” ambapo ameonekana akiwa amevalia crown yenye miiba, bastola kiunoni huku akiwa amembeba mtoto wake wa Kike. Mbele yake anaonekana mkewe Whitney Alford akiwa amekaa kitandani akimbembeleza mtoto wao mwingine. Album hii mpya itatoka chini ya lebo yake binafsi ‘PG Lang’ kwa ushirikiano na Top Dawg Entertainment. Ikumbukwe, “Mr. Morale & The Big Steppers” inaifuata albamu yake iitwayo “DAMN” iliyotoka mwaka 2017.

Read More
 RAPPER KENDRICK LAMAR KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE KWA WIMBO MPYA

RAPPER KENDRICK LAMAR KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE KWA WIMBO MPYA

Rapa kutoka nchini Marekani Kendrick Lamar ataikata kiu yako ya muziki muda wowote kuanzia sasa. Jarida la BILLBOARD limeripoti kuna uwezekano mkubwa wa Rapa Kendrick lamar kuachia wimbo mpya kati ya Februali 2 au 11 Kabla hajapanda jukwaani katika tamasha la Super Bowl Halftime Show. Tamasha hilo litawakutanisha maRapa kama Dr. Dre, Eminem, Snoop Dog, na linatarajiwa kufanyika Februari 13,mwaka huu wa 2022 Katika uwanja wa SoFi Stadium , California. Utakumbuka August 20 mwaka wa 2021 Kendrick Lamar alidokeza ujio wa album yake mpya baada ya ukimya wa miaka 4, album ambayo aliitaja kuwa ya mwisho chini ya label ya Top Dog Entertainment, ambayo aliitumikia kwa miaka 17.

Read More
 J. COLE ATHIBITISHA YEYE NDIYE ALIMSHAWISHI DR. DRE AMSAINI KENDRICK LAMAR

J. COLE ATHIBITISHA YEYE NDIYE ALIMSHAWISHI DR. DRE AMSAINI KENDRICK LAMAR

Rapa kutoka nchini Marekani J. Cole amefunguka na kusema kwamba yeye ndiye alimuweka Kendrick Lamar kwenye ramani ya muziki wa Hiphop. Kwenye mahojiano na mtangazaji Nardwuar, Cole amekiri kuwa yeye ndiye alimshawishi Dr. Dre amsaini Kendrick kwenye lebo ya muziki ya Interscope Records pamoja na Aftermath Entertainment mwaka wa 2012. Baada ya kuulizwa swali hilo na Nardwuar , J. Cole alisita kwa sekunde 15 na kushangaa kidogo kisha akasema“Ni nani amekwambia kuhusu hili? Ni nani amekupa hii taarifa? Jibu ni ndio. Nilifanya hivyo. Siwezi kusema mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumwambia, nilipomfikisha kwa Dre nilimwambia [Dre] unajua cha kufanya. Nampongeza Dre kwa uchaguzi sahihi.” Ikumbukwe Mwezi Machi mwaka 2012 Kendrick Lamar alisainiwa rasmi na Interscope Records pamoja na Aftermath Entertainment hivyo kuhitimisha safari yake ya kuwa msanii wa kujitegemea. Kazi yake ya kwanza chini ya label hiyo ilikuwa ni (good kid, m.A.A.d city) ambayo ni album yake ya pili.

Read More
 KENDRICK LAMAR MBIONI KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE

KENDRICK LAMAR MBIONI KUKATA KIU YA MASHABIKI ZAKE

Mkali wa michano kutoka Marekani Kendrick Lamar anaweza kudondosha album yake mpya kesho Ijumaa. Hii imekuja kufuatia kuvuja kwa ngoma iitwayo “Therapy Session 9” lakini pia mabadiliko ya picha ya Kendrick Lamar kwenye mtandao wa Spotify. Ni miaka minne tangu Kendrick Lamar asikike kwa upana kwenye masikio ya mashabiki zake kupitia album yake ya mwisho iitwayo DAMN iliyotoka mwaka 2017. Hivi karibuni alikuja na tamko la ujio wa album mpya na ya mwisho kwenye label yake ya Top Dawg Entertainment ambayo aliitumikia kwa miaka 17.

Read More