Mchekeshaji YY Aomba Msamaha Kwa Kutania Pesa Ambazo Kenrazy Anatoza Kwenye Show

Mchekeshaji YY Aomba Msamaha Kwa Kutania Pesa Ambazo Kenrazy Anatoza Kwenye Show

Mchekeshaji wa YY ameomba msamaha kwa kutania kiasi cha pesa ambacho mwanamuziki wa Kenya Kenrazy anatoza kwenye shows zake. Katika mahojiano na Plug TV, YY alinukuliwa akisema kuwa hawezimudu gharama za kumualika msanii Willy Paul kwenye shows zake kwa kuwa anatoza pesa nyingi ambapo alienda mbali Zaidi na kutania kuwa ni heri ampe show timmy tdat pamoja na kenrazy kwa sababu wasanii hao hawahitaji pesa nyingi kutumbuiza kwenye shows. “Kama tusipokuafford, tutaita Timmy Tdat na atakuja Hadi na Kenrazy na 40k.” Alisema. Kauli hiyo ilionekena kumkera kenrazy ambaye alitumia ukurasa wake wa instagram kusema kwamba yy alimvunjia heshima kwa kuidharau na kuishusha brand yake ya muziki ambayo ametengeneza kwa muda na pia ni brand ambayo imekuwa ikimuingiza kipato ambacho kimemsaidia kukithi mahitaji ya familia yake. “Nimekuwa nikijitahidi sana kutengeneza chapa yangu kila siku na hivyo siwezi kubali kauli kama hiyo inayotoka kwa mtu kama wewe. Kwa kweli  umenikosea sana, nilidhani unanijua vizuri zaidi. Unaniona nafanya kazi kila siku bila faida yeyote kutoka kwenye tasnia hii na kulea familia yangu kwa miaka hiyo yote, hivyo kukejeli sana yangu ni jambo lisilokubalika.”, Kenrazy aliandika kwa masikitiko. Hata hivyo Comedian YY alilazimika kumuomba radhi msanii kenrazy kwa kusema kwamba anasikitika kumtania Kenrazy na kumfanya ajisikie vibaya, kwani hakuwa na nia ya kujeli brand au chapa yake ikizingatiwa kuwa ni msanii mkubwa ambaye ameacha alama kwenye muziki wa Kenya.

Read More
 KENRAZY AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA CHAMA CHA KISIASA CHA ODM KISA MALIPO DUNI

KENRAZY AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA CHAMA CHA KISIASA CHA ODM KISA MALIPO DUNI

Staa wa muziki nchini Kenrazy amefunguka namna alivyolipwa malipo duni na chama cha kisiasa cha ODM wakati wa kampeni za urais mwaka wa 2013. Akihojiwa na Iko Nini, Kenrazy amesema alikuwa na matarajio makubwa kutoka kwa chama hicho kwani aliandamana nao kwenye kampeni zao nyingi. Hitmaker huyo wa “Mbilikimo Mkora” amesema licha ya kutumbuiza kwenye misafara tofauti za kampeini ya chama cha ODM alilipwa shillingi elfu 70 kwenye mkutano wa mwisho wa chama hicho katika bustani ya Uhuru. Rapa huyo amesema ‘malipo hayo duni’ yamemfanya kutofanya kazi tena na chama cha ODM ambapo amedokeza kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu atafanya biashara na chama kingine cha kisiasa ambacho kitamlipa vizuri

Read More
 KENRAZY ADOKEZA UJIO WA KAZI MPYA NA SOSUUN PAMOJA NA DUFLA DILIGION

KENRAZY ADOKEZA UJIO WA KAZI MPYA NA SOSUUN PAMOJA NA DUFLA DILIGION

Staa wa muziki nchini Kenrazy ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha Sosuun na Dufla Diligion. Rapa huyo mkongwe ametuweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushae picha ya pamoja na wasanii hao na kusindikiza na caption inayosomeka “SOSUUN x DUFLA DILIGON x KENRAZY Merry Christmas Everyone and STAY TUNED!!! LOADING…..” Ujumbe huo unoshiria kuwa mashabiki wakae tayari kwa ajili ya mfululizo wa nyimbo kutoka kwa wakali hao ambazo huenda zikatoka hivi karibuni. Ikumbukwe kazi ya mwisho iliyowaleta pamoja Kenrazy, Sosuun na Dufla Diligion ilikuwa ni wimbo uitwao Dawa ya moto ambao uliachiwa miaka 6 iliyopita chini ya lebo ya muziki ya Grapa Records

Read More