Duru ya Mwisho ya Raga 7s Kuwaka Moto Kisumu Wiki Hii

Duru ya Mwisho ya Raga 7s Kuwaka Moto Kisumu Wiki Hii

Msururu wa kitaifa wa raga ya wachezaji saba kila upande unatarajiwa kuelekea jijini Kisumu mwishoni mwa juma hili kwa raundi ya Dala, huku timu za KCB Rugby na Strathmore Leos zikitajwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kutawazwa mabingwa wa msimu huu. Mashindano haya yamepata msukumo mkubwa baada ya kupokea udhamini wa shilingi milioni 3 kutoka kwa kampuni ya Kenya Breweries, hatua inayolenga kuongeza morali na ubora wa mashindano katika hatua hii ya mwisho. Kwa sasa, KCB inaongoza jedwali kwa alama 104 baada ya kushiriki duru tano. Ili kujihakikishia taji la ubingwa, timu hiyo inahitaji tu kufuzu hadi robo fainali ya duru ya Kisumu. Upinzani mkali unatarajiwa kutoka kwa wapinzani wa kawaida kama Strathmore Leos na Menengai Oilers. Kundi A linajumwisha Kabras Sugar, CUEA Monks, MMUST na Nakuru RFC huku kundi B likijumwisha Daystar Falcons, MSC Rugby, Kenya Harlequin na Nondescripts. KCB Rugby, Mwamba RFC, Homeboyz RFC na Embu RFC wamo kundini C huku kundi D likihusisha Strathmore Leos, Menengai Oilers, Impala RFC na Kisumu RFC.

Read More