Msanii Parroty Aingia Kwenye Bifu Kali na Militan Baada ya Kunyoa Dreadlocks Zake Bila Ridhaa

Msanii Parroty Aingia Kwenye Bifu Kali na Militan Baada ya Kunyoa Dreadlocks Zake Bila Ridhaa

Msanii Parroty ameingia kwenye bifu kali na mwenzake Militan kufuatia tukio la kushangaza lililotokana na mzaha wa soka. Parroty, ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester United, awali alitania kuwa angenyoa dreadlocks zake endapo timu yake ingepoteza dhidi ya Tottenham. Baada ya United kufungwa 1-0, hali ilichukua mkondo mpya. Mzaha huo sasa umegeuka kuwa chanzo cha mgogoro mkubwa baada ya Militan kumvamia Parroty na kumnyoa dreadlocks zake bila idhini. Paroty, kupitia mitandao ya kijamii, alielezea hasira na kukerwa kwake na tukio hilo, akilitaja kama udhalilishaji wa hali ya juu. “Hii imevuka mpaka. Sio kila kitu ni mchezo. Sikutegemea nishambuliwe kwa sababu ya maneno ya mzaha,” alisema Paroty, akionya kuwa iwapo watakutana na Militan ana kwa ana, huenda mambo yakaenda kombo. Mashabiki wameingia kwenye malumbano, baadhi wakidai Parroty alipaswa kutimiza ahadi yake, huku wengine wakimtetea wakisema tukio hilo lilikiuka heshima na haki za mtu binafsi. Kwa sasa, Militan bado hajajibu hadharani, huku mvutano ukizidi kuongezeka na tasnia ya burudani ikisubiri kuona hatma ya bifu hilo linalozidi kushika kasi.

Read More
 Akothee Atangaza Kumsamehe Dada Yake Licha ya Maumivu ya Zamani

Akothee Atangaza Kumsamehe Dada Yake Licha ya Maumivu ya Zamani

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu wa Kenya, Akothee, amegusa mioyo ya wengi baada ya kushiriki ujumbe wa kihisia kwa dada yake, Elseba Awuor, akifichua kuwa amemsamehe na kuamua kuendelea na maisha bila chuki. Kupitia mitandao ya kijamii, Akothee aliandika ujumbe uliojaa hisia, akieleza kuwa msamaha wake haukutokana na ombi la dada yake, bali ni kwa ajili ya kutafuta amani ya moyo na kuondoa mzigo wa hasira alioubeba kwa muda mrefu. “Nimekusamehe, si kwa sababu uliomba msamaha, si kwa sababu ulirekebisha madhara hadharani, bali kwa sababu nastahili amani. Moyo wangu ni mzito mno kubeba hasira tena,” aliandika Akothee kwa hisia. Ujumbe huo mzito wa kihisia umeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki wake na wafuasi wa familia hiyo, wengi wakimsifu Akothee kwa kuchagua msamaha na kuponya nafsi yake badala ya kubeba chuki. Ingawa hakufafanua kwa kina yaliyotokea kati yake na dada yake Elseba, maneno yake yanaashiria majeraha ya kihisia yaliyomgusa kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, msanii huyo mwenye ujasiri amesema hatua hiyo ya kusamehe ni sehemu ya safari yake ya uponyaji na kutafuta utulivu wa ndani. Mashabiki na watu maarufu wamejitokeza kumpongeza kwa uamuzi huo, wakisema ni mfano mzuri wa ukuaji wa kiroho na kiakili. Wengine walimtia moyo kuendelea na safari ya upendo na mshikamano wa kifamilia, licha ya changamoto zilizopo. Akothee, anayejulikana kwa ujasiri wake wa kusema mambo bila kuficha, ameendelea kuwahamasisha watu wengi kuhusu umuhimu wa kuachilia chuki na kuchagua amani kama njia ya maisha

Read More
 Jovial Afunguka: Niliiba Taulo na Mashuka Ili Mtoto Apate Maziwa

Jovial Afunguka: Niliiba Taulo na Mashuka Ili Mtoto Apate Maziwa

Msanii nyota wa muziki nchini Kenya, Jovial, amefunguka kwa hisia kali kuhusu maisha magumu aliyowahi kupitia kabla ya umaarufu wake, akieleza kuwa aliwahi kuiba kwenye nyumba ya wageni (guest house) aliyokuwa akifanya kazi ili kumudu kulea binti yake mchanga. Kupitia Insta Story aliyochapisha jana kwenye mtandao wa Instagram, Jovial alisimulia kuwa wakati mmoja aliwahi kufanya kazi kama receptionist kwenye gesti moja huko Saba Saba, Mombasa, na kutokana na hali ngumu ya maisha, alilazimika kuiba mashuka na taulo kutoka gesti hiyo na kuyauza ili kupata pesa za kumtunza mwanawe aliyekuwa na umri wa miezi minne wakati huo. “Salo ilikuwa kidogo… a mother and child needed to survive. Tukibadilisha sheets na towels, usiku tunaiuza, tunagawanya hiyo doo Gai! Msinihukumu… Mungu hakutaka kuwe na CCTV juu singepata pesa ya maziwa ya mtoto.” aliandika Jovial. Jovial amesema kuwa, licha ya hayo yote, anakumbuka kwa shukrani hatua aliyopiga maishani na anajivunia kuwa mama ambaye hajawahi kata tamaa. Ameongeza kuwa kumbukumbu hizo humvunja moyo wakati mwingine, lakini pia humkumbusha kuwa bila matatizo hayo, hangejifunza kuwa imara na mwenye msimamo dhabiti kama alivyo leo. Jovial amewatia moyo mashabiki wake wanaopitia hali ngumu kwa sasa, akiwaambia wakae imara, kwani Mungu hutoa nafasi mpya kwa kila mmoja. “Cheki mtu akifanikiwa, usione kama hafai kuwa hapo… ni Mungu na yeye tu wanajua place ametoka!” Jovial alihitimisha kwa ujumbe kwa mashabiki na watu wanaopitia changamoto Kwa sasa Jovial anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki, na simulizi yake imewagusa mashabiki wengi ambao wameonyesha heshima kubwa kwa ujasiri wake wa kusema ukweli kuhusu maisha yake ya awali.

Read More