Keyshia Cole Amwaga Hisia Baada ya Kuvunjika kwa Penzi Lake na Hunxho
Malkia wa R&B, Keyshia Cole, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kuachana kwake na rapa Hunxho katika mahojiano mapya kwenye kipindi cha The Breakfast Club. Msanii huyo mashuhuri alizungumza kwa uwazi kuhusu hali yake ya sasa ya kimapenzi na kueleza kuwa bado hajapona kabisa baada ya kuvunjika kwa uhusiano huo. Alifafanua kuwa kwa sasa yuko single na kwamba hali hiyo si ngumu hata kidogo kwake. Hata hivyo, alikiri bado hajawa tayari kuanza mahusiano mapya, ingawa anapokea pongezi na ishara za kuvutiwa kutoka kwa wanaume wengine. “Niko single , siyo hali ngumu hata kidogo… ni kweli kabisa niko single,” alisema Cole kwa kujiamini. Keyshia alisema kuwa moja ya sababu zinazomfanya ajisikie bado hajawa tayari kuendelea mbele ni kwamba bado ana tattoo inayomkumbusha kuhusu Hunxho, jambo linaloonesha kuwa hisia bado zipo. “Sijaamua kurudi kwenye dunia ya mahusiano bado [lakini] napokea pongezi… lakini je, niko tayari kuendelea? Hapana. Bado nina tattoo hii hapa kwa hiyo siwezi… sijui,” aliongeza kwa hisia. Kauli zake zimewagusa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimpongeza kwa uaminifu na uwazi wake. Ingawa uhusiano wake na Hunxho umeisha, bado anaonekana kuugulia kimya kimya. Mashabiki wanaendelea kumuunga mkono na kumtakia afueni ya haraka na mafanikio katika maisha yake ya baadaye
Read More