Zuchu hana mpenzi wala mchumba -Khadija Kopa

Zuchu hana mpenzi wala mchumba -Khadija Kopa

Mama mzazi wa msanii Zuchu kutoka WCB Wasafi, Khadija Kopa amerejelea na kusisitiza kuwa mwanawe bado yuko singo na hana mwanaume yeyote awe mchumba au mpenzi. Kopa amesema kutokana na umaarufu wa Zuchu, siku akipata mchumba dunia nzima itajua na itakuwa ni habari ya mijini na vijijini, ila kwa watu wawe na subira na kutopotoshwa na kile ambacho wamekuwa wakikisikia mitandoani na kwenye mablogu ya udaku. “Zuchu bado yupo single, hana mpenzi wala Mchumba na wala hajanitambulisha kwa Mwanaume yoyote kwamba Mama huyu ndiye Mwanaume wangu, Zuchu ni maarufu hata mimi Mama yake ni maarufu siku atakapopata Mchumba akanitambulisha matajua tu muwe na subira,” alisema Khadija Kopa. Ikumbukwe Zuchu anatajwa kuwa na mahusiano na Diamond Platnumz lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha hilo, ila mitandaoni wanaonekana kama wapenzi.

Read More
 Khadija Kopa achukizwa na ujumbe wa kaka yake Diamond

Khadija Kopa achukizwa na ujumbe wa kaka yake Diamond

Malikia wa mipasho Tanzania Khadija Kopa ambaye pia ni mama mzazi wa nyota wa muziki wa bongo fleva Zuchu, ameonesha kuchukizwa na ‘Komenti’ ya Romy Jons ambayo aliiandika kwenye ukurasa wa Instagram wa Zuchu. ‘Komenti’ hiyo iliandikwa baada ya Zuchu kuposti picha zake akita amevaa ‘Taiti fupi’, Romi aliandika, ‘’SHAPE NDIO HUNA MWAYA’. Kupitia ‘komenti’ hiyo Khadija Kopa alishindwa kuvumilia na kuamua kutoa neno kumtaka Mwanae asiende Uturuki ambapo wengi huwa wanaenda kufanya upasuaji ili kuongeza umbo. Khadija aliandika, ‘’Wala usiende Uturuki mwanangu alonacho yeye huna na ulonacho wewe yeye hana huyo ndio Mungu @romyjons’’ Ikumbukwe kuwa Romy amekuwa mtu wa utani mwingi katika mitandao ya kijamii hasa katika komenti zake ambazo huwa anaandika kwa baadhi ya kurasa za watu mbalimbali.

Read More
 BI KHADIJA KOPA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMUANDIKIA MWANAE ZUCHU UJUMBE MZITO

BI KHADIJA KOPA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMUANDIKIA MWANAE ZUCHU UJUMBE MZITO

Mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Tanzania Bi Khadija Kopa ambaye ni mama mzazi wa msanii kutoka WCB Zuchu Ameweka ujumbe ambao umewaacha watu wengi na maswali mengi katika mitandao yake ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Khadija Kopa amendika Ujumbe wa kumtakia kheri mwanae Zuchu katika maisha yake mapya ambayo yataanza siku ya Valentine  Februari 14 ambapo amesema kila mwanamke ana ndoto ya kuishi maisha hayo. “Zuhura mwanangu Nimekulea kwenye maadili na Najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti .Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asie na ndoto hii.M/Mungu akakusimamie najua hutoniangusha .siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndo mwanzo wa maisha mapya yenye Furaha .M/Mungu Akulinde kiziwanda changu Amin” ameandika Bi Khadija Kopa. Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameibuka na kuhoji kuwa huenda siku hiyo zuchu akavishwa pete ya uchumba na bosi wake diamod platinumz ambaye katika siku za hivi karibuni amehusishwa kutoka kimapenzi na hitmaker huyo wa “Sukari. Wengine wameenda mbali Zaidi na kusema kuwa huenda Zuchu akaachia album au E yake mpya siku hiyo ya wapendanao duniani ila ni jambo la kusibiriwa.

Read More
 KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

KHADIJA KOPA AVUNJA KIMYA CHAKE KUHUSU ISHU YA DIAMOND KUTOKA KIMAPENZI NA ZUCHU

Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki diamond platnumz kutaka kumuoa mwanamuziki mwenzake zuchu , sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake. Sasa mama mzazi wa zuchu, Khadija Kopa amezungumzia kile kinachoitwa penzi jipya mtandaoni kati ya binti yake, Zuchu na Diamond Platnumz. Kwenye mahojiano Kopa  ambaye ni Malkia wa muziki wa Taarab nchini tanzania amepuuzilia mbali madai hayo na kusema aliwasiliana na bintiye na akamueleza hali halisi kuwa huo ni uvumi tu usio na msingi. Zuchu alimhakikishia mama yake kuwa Diamond amekuwa akimuonyesha heshima kubwa na hakuna chochote kinachoendelea kati yao. “Wakati ule Zuhura aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku moja kuniambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maanake watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi” amesema na kuongeza; “Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi, mimi mwenyewe sikushughulika sana, nilimuuliza Zuhura mbona watu walivumisha sana ama kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja, mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida” alisema Khadija Kopa. Aliendelea kwa kusema; “Diamond mimi ananiona kama mama yake kusema ukweli, tangu zamani, kabla hata huyo Zuchu hajaenda Wasafi, amenichukulia kama mama yake”.

Read More