INVISIBLE CURRENCY ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YATUMIKA KAMA COVER YA NEW YORK TIMES BILLBOARD YA NCHINI MAREKANI
Rapa Khaligrph Jones anazidi kuchana mbuga kimataifa hii baada ya cover ya album yake mpya iitwayo “Invisible Currency” kutumika kama art work ya chati ya New York Times Billboard ya nchini Marekani. Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones amewataarifu mashabiki zake taarifa hiyo njema kwa kushare picha ikionyesha picha yake ambayo ilikuwa imechapisha kwenye chati ya new york times square billboard huku akiwashukuru mashabiki zake ambao wamemshika mkono hadi akafikia mafanikio hayo. Hata hivyo Khaligrph Jones anakuwa msaani wa pili kutoka Afrika Mashariki album yake kutumika kama cover kwenye chati hiyo kubwa ya muziki nchini marekani baada Bahati ,Azawi, Rayvanny, Mbosso na Eddy Kenzo. Ikumbukwe New York Times Billboard wamekuwa na utaratibu wa picha za mastaa wa muziki ambao ngoma zao zinaongoza kwa mauzo kwenye mitandao mbali mbali ya kusikiliza muziki duniani.
Read More